Home

Thursday, November 10, 2011

Nibebe Lyrics - Rose Muhando


Rose Muhando
Album Jipange Sawa Sawa
Artistes Rose Muhando
Language Swahili
Writer Rose Muhando
Year 2008

(chorus)
Nibebe nibebe nibebe nibebe
Nibembeleze nibebe
Nichukue unibebe
Mikononi mwako niwe salama

(verse1)
E mungu angalia kunena kwangu,
Na usikie sauti ya kilio changu
Moyo wangu umechoka sana baba,
Kwa ajili ya wingi wa mateso yangu
Nafsi yangu imegandamana na mavumbi
Niokoe mikononi mwa midomo ya mbwa
Kwanini ninateswa sana kwa ajili yako babaga
Niokoe mikononi mwa watu wabaya
fanya hima unisaidie nibebe

Chorus
Nimechoka peke yangu safari ngumu no ndefu nibebe
chorus

(verse 2)
Macho yangu yamedhoofukwa machozi
Kwani mateso yangu hayapimiki kwa mizani
Kwa kuwa aliyenitukana siye adui yangu
bali ni rafiki yangu tuliyejuana naye sana
Tulikula pamoja, tulisali pamoja, kanisani pamoja
Bwana asifiwe kwa sana
Kumbe mwenzangu alikusudia kuniangamiza

chorus
Kweli nimeamini adui wa kwanza ni yule wa nyumbani mwako
chorus

(verse 3)
Wengine wakinibeba nitaambulia matatizo, yesu nibebe
Dunia ikinibeba itanipeleka jehanamu, yesu nibebe
Marafiki wakinibeba watanipeleka pabaya, yesu nibebe
Baba nibebe, yesu nibebe,
Nibembeleze nibebe, nichukue mbiguni salama

chorus
Nimechoka pekee yangu safari ngumu siwezi
chorus

(verse 4)
Nifike mbinguni nimwone Eliya (Amen)
Nifike mbinguni nimwone Yakobo (Amen)
pamoja na kiti cha enzi mbinguni kwa baba
Njia za dhahabu nami nakatembelee
O baba nibebe, yesu nibebe,
Nibembeleze nibebe, nichukue mbiguni salama

chorus
Nakwita Yesu unibebe mwokozi
Chorus

(verse 5)
Nifike mbinguni nikamwone baba (Amen)
Nifike mbinguni nakapumzike (Amen)
Katika kiti cha enzi nami nikasujudie
Niwaone wenzangu wale walionitangulia
Nikale matunda ya mti wa uzima
Yesu nibebe, baba nibebe,
Nibembeleze nibebe nichukue mbiguni salama
Chorus

No comments:

Post a Comment