Home

Thursday, November 3, 2011

Package From Altar:JIFUNZE KUOMBA KWA NIDHAMU YA “MUDA WA KUOMBA” 1.



Nakusalimu kwa jina la Bwana.

Imenilazimu  katika mwezi huu tuweze kujifunza jambo hili juu ya “kuomba kwa kuzingatia muda wa kuomba”. Maombi ni somo pana sana, ndani yake kuna vitu vingi sana ambavyo kila siku Roho matakatifu yuko tayari kutufunza kwa kila aliye tayari kujifunza.

Hebu leo tujifunze kwa shuhuda kadhaa;

Ushuhuda wa kwanza;
Tarehe 18/09/2008, nikiwa mkoa wa Dare s salaam nilikaribishwa nyumba fulani kwa chakula cha jioni na kupumzika hapo. Kwa kawaida mimi ni mpenzi sana wa kuangalia kanda za video za vita. Baada ya chakula cha jioni mtoto mmoja wa ile familia akaniwekea mkanda wa vita niliouchagua. Basi tukaanza kuangalia huku tunazungumza mambo kadha wa kadha. Kama wewe ni mpenzi pia wa kanda hizo utagundua nyingi zake huwa zinaanza na kisa fulani halafu mbeleni ndio kunakuwa na mapambao mazuri kweli kweli, (mniwie radhi msiopenda kanda za vita, maana najua mpo) nimelazimika kutumia ushuhuda huu ili ujumbe uweze kueleweka.

Sasa mkanda ulipofika mahali ambapo ni patamu au pazuri kwa maana ya mapigano kuanza ghafla nikasikia rohoni msukumo wa kuomba uliokuja kwa kasi ya ajabu. Nikajaribu kujivuta vuta ili mkanda uishe kwanza, msukumo ukazidi kana kwamba utafikiri kuna mtu anachochea jiko, (ndani niilijua nini natakiwa kufanya lakini akili ilikuwa kwenye mkanda). Nikamwambia Roho mtakatifu niache nga nimalizie mkanda ndio nikaombe. Ghafla nikaletewa kwenye ufahamu wangu picha ya watu katika nchi fulani wanaoteseka na kuuwawa kwa sababu ya kumwamini Yesu. Ndipo likaja swali huo mkanda na hizi roho za watu walioniamini kipi muhimu?


Nakumambia licha ya kwamba nilikuwa ugenini nikamwambia yule ndugu niruhusu nikitumie chumba chako kuomba kwa muda usiojulikana. Niliingia kwenye maombi usiku ule bila kujali nipo ugenini maana rohoni nashuhudiwa usipoomba kuna roho zinaangamizwa usiku huu. Niliomba maombi ya kumanaisha mpaka nilipoona shwari rohoni mwangu. Nilipomaliza nakumbuka ilikuwa kama saa sita  hivi, hapo ndipo nikarudi kwenye kideo sasa, kwa raha zangu niliangali hadi saa nane. Nasema ka raha zangu kwa sababu ule msukumoulkuwa umekwisha saa hiyo. 

Baada ya hapo tukaenda kulala kulipokaribia kucha ndipo Roho wa Yesu akanionyesha kitu kilichotokea wakati waombaji wengine nikiwemo na mimi tulipokuwa tukiombea ile nchi. Maana najua jambo hili Mungu aliweka kwa watu wengi siku ile na ndio maana nimeandika na tarehe kabisa. Kristo akanishuhudia kwamba kwa kutii kule tuliubariki  sana myo wake. Nikamshukuru na kuendelea na kazi za siku hiyo.

Ushuhuda wa pili;

Siku moja, Ijumaa asubuhi, wakati najiandaa kwenda ofsini ghafla ukaja msukumo ndani yangu wa kumuombea kijana mmoja ninaye mfahamu, maana alikuwa ana kesi fulani mahakamani na Jumatatu ya wiki iliyofuata ndiyo ilikuwa hukumu yake. So nilichokifanya nilitii agizo la Mungu nikaanza kuomba, nikaomba kwa muda kiasi na kisha nikaendelea na kazi zangu za siku ile. Ilipofika Jumatatu yule ndugu akaenda mahakamani, kumbe kwa bahati mbaya alichanganya tarehe alitakiwa kwenda ile Ijumaa na siyo Jumatatu. 

Na kwa sababu hiyo mshtaki wake akawa amepewa kibali tangu Ijumaa cha kumkamata lakini ahsante kwa Yesu hakufanya hivyo, na baada ya taratibu nyingine za kimahakama kufuatwa wakapangiwa tarehe nyingine ya kufika mahakamani

Na Patrick Sanga

No comments:

Post a Comment