Home

Tuesday, December 27, 2011

GOSPEL FESTIVAL 2011 YATIKISA MWANZA

Mgeni rasmi aliyemwakilisha mkuu wa mkoa wa Mwanza Diwani wa Mkolani Stanslaus Mabula akimkabidhi Mtumishi wa Mungu Dr. Moses Kulola Cheti kutambua mchango wake katika muziki wa Injili.
Kwaya
Marafiki waalikwa, hapa ilikuwa mwanzo kabisa katika Tamasha hilo kubwa la aina yake lililofanyika leo jioni Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza .
Mwimbaji wa Muziki wa Injili nchini Tumsifu Rufutu akiwa katika vazi la Musa akiinyoosha fimbo yake kuigiza tendo la kuitenganisha watu mithili ya bahari.
Tumsifu Rufutu aka Musa akiwaongoza wahudhuriaji aka wana wa Israel..
Mara safari ya kuelekea Kaanani kupitia wimbo wake maarufu mwambie Farao ikawadia..
Wageni wetu walio hudhuria tamasha hilo la kwanza lijulikanalo kwa jina la Gospel Festival 2011.
Wageni ni kuimba na kusifu.
Mgeni rasmi aliyemwakilisha mkuu wa mkoa wa Mwanza Diwani wa kata ya Mkolani Stanslaus Mabula akimkabidhi cheti Mtumishi wa Mungu Bishop Charles Sekelwa kwa mchango wake wa kuendeleza muziki wa Injili.
Mtumishi wa mungu Bishop Zenobius Isaya akionyesha cheti alichotunukiwa na Kampuni ya F Plas Intertainment kuthamini mchango wake katika kukuza muziki wa injili.
Mapambano Kwaya kutoka Geita...

Vijana Anglican Nyamanoro Choir wakipata flash ya pamoja.
Wakongwe Aic Makongoro Kwaya nao wakipata flash ambapo hii ni moja kati ya kwaya zilizo tunukiwa cheti maalum kwenye tamasha la Gospel Festival 2011.
Ni fursa ya Moja kati ya Wadhamini Winning Shoping Centre akitangaza huduma zao kwa umati uliohudhuria tamasha hilo pembeni yake amesimama Meneja mipango wa F. Plus Intertainment Albert G. Sengo
Mwimbaji Daniel Safari (R) na (L) wakiwa na mkurugenzi wa F Plus Intertainment Fabian Fanuel (C)
 
Souce:Gsengo

No comments:

Post a Comment