Home

Wednesday, December 7, 2011

Kirk Franklin amaliza ziara yake Barani Africa


Kirk Franklin
Mwanamuziki wa injili kutoka nchini Marekani Kirk Franklin Tarehe 5 DEC 2011 amefanikiwa kufanya Tamasha la Muziki wa injili nchini Zambia. Katika tamasha hilo lililohudhuriwa na umati wa watu, Kirk kabla ya kufanya tamasha nchini zambia alitokea Nchini Nigeria ambako walifanya tamasha siku ya Ijumaa tarehe 2 Dec 2011. Kirk mwenye miaka 41 baada ya Concert la nchini Zambia alielekea Harare nchini Zimbabwe kwa Concert lingine lililofanyika jana Tarehe 6/12/2011.

Wakati alipowasili katika uwanja wa Ndege wa Keneth Kaunda jijini Lusaka, Kirk aliwaambia waandishi wa habari kuwa “ moja kati ya maazimio ya Ziara hiyo ni pamoja na kuangalia uwezekano kufanaya kazi na wanamuziki wa injili wa nchini humo ili kuwasaidia katika kutimiza ndoto zao.

See Below Kirk Franklin in Zambia

 

No comments:

Post a Comment