Home

Wednesday, February 29, 2012

Mtoto wa Nabii GeorDavie aitwaye Nisher atoa shukrani kwa Baba yake


Nisher
Nisher ni mtoto wa Mtumishi wa Mungu Mh Nabii GeorDavie anayeongoza huduma ya Ngurumo ya Upako yenye makao yake jijini Arusha. kwa muda sasa Nisher amekuwa akijihusisha na muziki(Gospel and Non Gospel Music),toka mwaka huu uwanze ndoto yake ya kuwa na studio kubwa kwa ajili ya kurekodia aina zote za Muziki imekamilika na sasa anamiliki studio ijulikanayo kama NISHER RECORDS iliyoko jijini Arusha.

Kipekee nimeanza kumfahamu Nisher takribani miaka mitatu iliyopita nikiwa mwaka wa pili chuoni pale St Augustine Univ, na hii ni baada ya kuona quality ya Video production ya Ziara na huduma za Nabii Geordavie,nilipouliza who is behind this  unique art nikaambiwa ni mwanaye anaitwa Nisher.Unaweza mjudge Nisher vyovyote but pamoja na hayo Nisher is Talented, hufanya Graphics za viwango vya juu kuanzia Video mpaka Photo Pictures

Baada ya studio yake kuanza kazi studio jijini Arusha huku ikigharimu Kwa haraka haraka zaidi ya 15M inadeal na Video na AUDIO,kwa kutambua mchango wa Baba yake katika maisha yake na katika mafanikio yake Nisher aliamua kurekodi Mini Video Clip kwa ajili ya kumshukuru baba yake kwa hatua aliyomfikisha. Katika Video Clip hiyo, Nisher anasema mafanikio yake yote yanatokana na baba yake.

Nisher akiwa ndani ya Nisher Records
Akasema”Nisher records it has been possible because of my daddy,My Daddy alinisaidia ku-put kila kitu Together Financially pamoja na kwenye maduka (katika kuchagua vyombo) kwa kuwa amekuwana historia kubwa na muziki kuliko mimi,amekuwa akifanya Muziki kwa zaidi ya Miaka Arobaini sasa.Namshukuru sasa baba kwa kunisaidia na kwa kuona kuwa i can do better, i can be a better person, napenda kukushukuru Honestry mbele ya watu wote wanaoangalia Video hii kwamba your my HERO and God Bless you for that, naamini Nisher Records and Nisher Entertainment it will be Big Company” 

Katika Maisha ya wokovu,watu wengi waliookoka huwa wako mstari wa mbele katika kukosoa na kulaunu namna watoto wa watumishi wanavyoishi na namna wanavyouchukulia wokovu.Kwa upande wa pili kanisa linasahau wajibu wake kwa vijana na kubaki kuwalaumu na kuwafanya ndio Hot topic popote pale hususani wanapotoka nje ya mstari.Pamoja na yote hayo Mungu anabaki kuwa Mungu kwa kuwa Habadiriki, na kanisa lapaswa kusimama na kuwaombea watumishi  pamoja na familia zao pasipo kuwanena vibaya.


Milca L. Kakete mtanzania anayemtumikia Mungu nchini Canada


Milca L. Kakete
Leo hapa katika Hosanna Inc hususani kwenye safu ya “watanzania watumikiao Mungu nje ya Tanzania” tunaye Milca Kakete. Milca L. Kakete ni Mtumishi wa Mungu kutoka nchini Tanzania na kwa sasa anamtumikia Mungu nchini Canada.Baada ya kuurekodi na kuutoa wimbo wa NATAMANI,wimbo huu ulimtambulisha vizuri Milca katika vinywa vya watu wengi hapa nchini.

Natamani Kufanana Nawe
Natamani Kufanana Nawe
Sikuzote za Maisha yangu

Hapa Milca anaelezea historia yake na utumishi wake kwa ujumla.

Milca Kakete:Napenda kuchukua nafasi hii kushukuru kwa mwaliko huu wa kushiriki ambayo Mungu ameandaa.

Historia yangu kwa kifupi mimi ni mtoto niliyezaliwa katika familia ya wazazi waliompokea Yesu maishani mwao, nikiwa na umri mdogo sana niliimba Kanisani na hatimaye kuanza kurekodi na kwaya moja ya Nkinga Christian ya huko Tabora nilishiriki kuimbisha nyimbo kadhaa katika album yao mojawapo.

Mwaka 2003 Mungu aliongea nami kutoa kanda ya nyimbo za kuabudu inayoitwa "Yesu niko mbele zako" inayobeba nyimbo kama "Natamani,na Nifinyange"

Nampa Mungu sifa kwa matendo makuu aliyotenda kupitia kanda hiyo, maana nilipokea ushuhuda wa ndugu mmoja aliyekuwa ana maombi juu ya uponyaji wa ugonjwa aliokuwa nao,na akiwa ndani ya chumba chake aliambiwa na Mungu asikilize kanda hiyo baada ya muda alizimia na alipoamka aliambiwa amepona ugonjwa huo ulikuwa ukimwi na akaenda kupima amepona.

Milca L. Kakete akiwa na Mwanaye
kanda hiyo itakuwa madukani kwa mara nyingine tena miezi ya karibuni. pia kuna kanda nyingine ambayo sikuitoa madukani ila ni ya zamani kidogo.
na nyingine itakayokuwa iko sokoni hivi karibuni pia inayoitwa "Mwanangu Njoo". Jumla ni kama kanda 3 ambapo moja iliyokwisha toka na mbili bado hazijatoka na baadaye Mungu alinileta nchi ya Canada ambapo namtumikia Mungu.

Milca Kakete akiwa na Mume wake Kakete Sephan

Hosanna Inc:Kuna tofauti gani  kati ya kumtumikia MUNGU ukiwa nchini Tanzania na uwapo nchini Canada?

Milca:Tofauti nayoiona kati ya utumishi wa nyumbani Tanzania na huku kwa wenzentu ni mambo kadhaa

Moja, ni kwamba hapa hakuna uhuru wa kutoa mashauri kwa mtu binafsi kirahisi hata kama unaona mtu anahitaji msaada tofauti na nyumbani na hii nadhani ni kutokana na "maendeleo" ya teknolojia,teknolojia huja na mambo mengi ambayo hubadilika na kuwa ufungwa uliofichika ambapo adui anatumia maendeleo kuweza kuondoa nafasi ya Neno la Mungu kupenya kirahisi kwa watu.

Pili,ni swala la uthamani na umuhimu wa familia kwa kwa hapa adui kapata nafasi kubwa kufarakanisha familia, na waathirika ni watoto zaidi maana utengano wa familia unapotokea mtoto hana uchaguzi hata kama angependa wazazi wote wawe pamoja ili aendelee kufurahia upendo wa familia na baada ya hapo anaanza kukua akiwa na athari kisaikolojia mpaka huenda kufikia maamuzi mabaya ya maisha yake na hatimaye kuharibu maisha kabisa na hapo ndipo adui anapopataka maana mwisho wake ni kubadili kizazi kutoweza kuwa na maadili mema.

Hosanna Inc: Unaushauri gani kwa watumishi wa Mungu mbalimbali?

Milca:Maoni yangu juu ya watumishi wa Mungu ni kuwa waangalifu jinsi tunavyoipokea teknolojia hii maana inakuja na vishawishi vilivyojificha sana ambavyo adui anavitumia kupungua focus ya huduma zetu na kukalia vitu ambavyo viko nje ya mpango wa Mungu.Ni muhimu sana kuwa katika maombi juu ya huduma zetu zote maana vita tuliyomo inahitaji silaha kubwa zaidi ambayo maombi tu huweza kushindwa yote.




Her  favourite Colour 
 Brown
Her Favourite Hymn(Tenzi) 
 Naupenda Msalaba Huu
Nje ya uimbaji 
 Mimi ni mama ushauri na mwalimu wa wanawake
Her Best Bible verse 
Yeremia 29:11( Maana nayajua mawazo ninayowawazia...)


                                    Mungu awabariki

Milca L.Kakete


Tuesday, February 28, 2012

Ni Lazima Ushinde :Pastor Eliud Mwasenga


Pastor Eliud Mwasenga

Luka 8: 40-50
Katika mistari hoyo tunamuona Yairo, aliyekuwa na binti yake mgonjwa na kuamua kutafuta msaada toka kwa Yesu.Wakati anamwambia Yesu Matatizo yake kwa namna ambavyo Yesu alikuwa akimjibu alifikiri labda Yesu hatilii maanani tatizo lake.Na wakati huo huo Yairo akaletewa habari kutoka nyumbani kuwa Binti yake amefariki. Alipomwambia Yesu mtoto amefariki Yesu akamwambia MTOTO HAJAFARIKI.

Unaweza kuona namna ambavyo mazingira yanasema wazi kuwa mtoto amefariki lakini Yesu anapingana na Mazingira hayo. Hata siku moja usiyatii Mazingira ila amini katika kile Yesu asemacho juu ya Mazingira hayo. Kwanza unatakiwa kuchagua kuamini katika Neno la Mungu inawezekana ni kweli kabisa umefeli mitihani darasani, au biashara haiendi vizuri, au mwili haujisikii vizuri kisha kumbuka kile ambacho Mungu amesema juu ya eneo hilo na ndicho ukitamke.

Ebrania 12: 1 Kwa kuwa tumezungukwa na mashahidi wengi, katika yale tunayoyafanya japokuwa ni changamoto kwetu lazima tujue kuwa tumezungukwa na mashahidi wengi ambao wanakutarajia wewe ushinde ili nawao waweze kupenya kwenye maeneo yao, Hivyo ni Lazima ushinde. Haijalishi unapitia wapi na nini, chagua kutomungusha Mungu kwa kuwa anategemea wewe ushinde.

Yezeberi alimtisha Eliya kwa kumwambia kuwa atamuua, na Eliya hofu ilimjaa akatishika na akaamua kwenda kujificha mapangoni ili asikutane na mkono wa Yezeberi. Alipokuwa yuko pangoni Mungu alimwambia toka huko.Na hivi leo Mungu bado anasema toka kwenye hali uliyonayo kwa kuwa mimi nipo kukupa msaada.

Wakati Goliath aliposimama na kuanza kulitukana Jeshi la Mungu, Daud hakukaa kimya, japokuwa Goliath alikua tishio kwa wayahudi wote, lakini pindi alipoanza kutukana Daudi alikumbuka Matendo makuu ya Mungu na hivyo hakukaa kimya akasema wewe ni nani hadi utukane majeshi ya Mungu aliye hai.Hivyo wakati uko vitani sema na kumbuka ukuu wa Mungu kwa kuwa katika hiyo vita uliyopo Mungu anatarajia Lazima Uishinde kwa kuwa yeye yuko upande wako.

 
Pastor Eliud Mwasenga.

Brazili yawa nchi ya pili Duniani kwa kutoa idadi ya wamishinari wengi kwenda miisho ya dunia


Mnara mkubwa kabisa wa YESU duniani ulioko katika jiji la Rio De Jeneiro nchini Brazili
Nchi ya Brazili imekuwa ni nchi ya pili duniani kwa kutoa idadi kubwa ya wamishionari wanaokwenda sehemu mbalimbali duniani kwa lengo la kumtangaza Kristo. Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na taasisi ya kimarekani ijulikanayo kama Global Christianity study Organisation, Brazili ilitoa jumla ya wamishionari wapatao 34,000 kati ya jumla ya wamishionari 400,000 waliotumwana mataifa yote duniani kwa mwaka 2010.

Katika utafiti huo wakati Brazilli ikichukua nafasi ya pili, Marekani yenyewe ndio inaongoza kwa kutoa jumla ya wamishionari 127,000.Pamoja na Marekani kuongoza,Marekani pia imekuwa nchi ya kwanza katika kupokea idadi kubwa ya wamishionari kutoka mataifa mengine wanaoingia nchini humo kwa ajili ya kumtangaza Kristo Yesu.

Kwa mwaka 2010 Marekani ilipokea jumla ya wamishionari wapatao 32,400 na wengi wao wakitokea nchini Brazili.Kwa sasa Brazili ni nchi ya pilli duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya wakristo wa madhehebu ya Kiprotestant.

Kwa sasa idadi ya wamishionari wa kujitolea imeongezeka kwa kasi dunuani hususani baada ya kuongezeka kwa teknolojia ya Mawasiliano ya uma(Teknohama), ambapo mtu anaweza kukaa nyumbani kwake na kuhubiri au kuhubiriwa kwa njia ya Internet. 

Mtumishi Atosha Kissava kutoka Iringa kushiriki tamasha la Pasaka Mwaka huu


Atosha Kissava

TAMASHA la Pasaka linalofanyika kila mwaka kwa kuandaliwa na Kampuni ya Msama Promotions ya Dar es Salaam, linazidi kupanuliwa wigo mwaka huu kwa kushirikisha wasanii nguli na wanaoinukia.

Akizungumza na mwanahabari wa jambo leo jijini Dar es Salaam jana, Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama alisema mwimbaji Atosha Kissava kutoka Mkoa wa Iringa amekuwa wa tatu kuthibitisha kushiriki tamasha hilo. "Kissava ambaye ana kundi lake la muziki wa injili, anakuwa mshiriki wa tatu kuthibitisha kushiriki tamasha la Pasaka baada ya Upendo Kilahiro na Upendo Nkone," alisema Msama.

Tamasha hilo linatarajiwa kurindima Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Aprili 8 mwaka huu na pia litafanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Aprili 9 mwaka huu. Kissava hivi sasa anatamba na albamu ya Nainua Macho Yangu Juu yenye nyimbo za Alpha na Omega, Unaweza, Nifanane na Wewe, Nibariki na Mimi, Kwake Yesu, Njooni Njooni, Yatima na Nainua Macho uliobeba jina la albamu.

"Tunaboresha mambo mengi kuliko miaka iliyopita, waimbaji mwaka huu watakuwa wachache kiasi wakiwamo wa kutoka mataifa mengine ya Afrika... hiyo yote tumefanya ili kukidhi matakwa ya wapenzi wa muziki wa injili. "Mbali na Tanzania, pia tutakuwa na waimbiaji kutoka Kenya, Uganda, Zambia, Afrika Kusini, Rwanda na Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo katika tamasha hilo la nyimbo za injili za kumsifu Mungu.

Picha Yetu Jumatatu Hii:Benjamin Dube akiwa na Bishop Thomas Jakes


Pichani anaonekana Kiongozi wa Kanisa la Potters House la nchini Marekani Askofu Thomas Jakes(TD Jakes) akiwa familia ya Baba na Mama Mchungaji Benjamini Dube wa nchini Afrika ya Kusini.

SAUT Wamwadhimisha Bwana katika Campus Night


Lile Tamasha la kusifu na kuabudu lililokuwa likisubiliwa kwa hamu na wanachuo na wakazi wa Mwanza lijulikanalo kama campus Night, ijumaa iliyopita lilifanyika  katika viwanja vya shule ya msingi Nyamalango iliyoko Nyegezi jijini Mwanza  karibu kabisa na Chuo kikuu cha Mtakatifu Augustine(SAUT).Vikundi kama TAFES SAUT,KingDom Worshipers,CASFETA,HHC Praise and Worship Team pamoja na kihaire Band vilimuadhimisha Bwana Viwanjani hapo.

Maandalizi ya  Tamasha hilo yalifanyika  kwa ushirikiano mkubwa kati ya TAFES-SAUT na kanisa la HIGHWAY OF HOLLINES  linaloongozwa na Akofu Eugine Mulisa. Tofauti na Matamasha mengine Tamasha hili lilikuwea la kihistoria kwa kuwa lilikuwa ni tamasha la kwanza kurushwa LIVE kupitia kituo cha redio cha  ALIVE FM ambapo Nyamiti Kanyola mmoja wa watangazaji wa redio hiyo aliongoza jopo la ufundi kutoka ALIVE FM katika kuhakikisha walioko majumbani wanakutana na ngumu za Mungu.

Mtumishi wa Mungu Askofu Eugine Mulisa akifundisha Neno la Mungu kisha akaongoza idadi kubwa ya watu sala ya toba  baada ya kuamua kumpokea YESU kama Bwana na mwokozi wa Maisha yao.Tofauti na Campus Night zilizowahi kufanyika na Maombezi kuwa ni sehemu tu ya Mahubiri, kilichojiri kwenye Concert hili ni Tofauti kwani waliolipuka Mapepo walikuwa ni wengi mno hivyo kupelekea wahudumu na watumishi kuwa na kazi ya ziada katika kufanya huduma ya Maombezi.
Evelyn Andrew New member wa bend ya KingDom Worshiper na mtangazaji wa Kwa Neema Fm akiwa on stage.

Tafes Saut Praise and Worship Team ikihudumu



Mtumishi wa Mungu Askofu Eugine Mulisa akifanya maombezi

Maombezi yakiendelea



Watumishi wakiendelea na maombezi




Kingdom Woshipers on Stage

Friday, February 24, 2012

Mchungaji Boazi Sollo Kuunguruma Mbeya

Boaz Sollo
Mtumishi wa Mungu Boaz Sollo kwa sasa amekuwa akisikika sana katika masikio ya watanzania hususani walio karibu na Media, mchungaji Sollo ni kiongozi wa kanisa la lijulikanalo  kama EndTime Harvest Church lenye makazi yake mkoani Iringa. Amekuwa akihubiri injili katika sehemu mbali mbali na hivi karibuni alifanya mkutano wa injili mkoani Dodoma.

Mchungaji Sollo alimpokea Yesu kama Bwana na mwokozi wa Maisha yake mnamo mwaka 1997 na baada ya kuukulia wokovu amekuwa akifundisha na kuhubiri sehemu mbali mbali nje na ndani ya Tanzania.  Kwa upande wa elimu Mch Sollo ni Mhitimu wa shahada ya Theolojia katika chuo kikuu cha Breakthrough Bible College kilichoko nchini Marekani.

Mungu amekuwa akimtumia Mch Sollo kwa ishara kubwa na maajabu ambapo katika mikutano yake na Ibada kanisani kwake watu wengi wamefunguliwa kwa uweza wa Mungu.Tofauti na kuhubiri Mchungaji Sollo ni ni mwandishi na Muimbaji wa nyimbo za injili ambapo mpaka sasa amesharekodi jumla ya Album za muziki wa injili zipatazo tatu.

Kwa sasa  Mtumishi Sollo anajipanga kufanya mkutano mkubwa wa injili jijini Mbeya Kuanzia tarehe 9-03-2012 mpaka tarehe 11-03-2012 katika Viwanja vya Uhasibu. Tunaamini kuwa Yule Mungu aliyeianzisha kazi ndani yake atatokea na kuikamilisha kwa utukufu wake.

Thursday, February 23, 2012

Mtumishi Freddy Chavala Kuanza Season One Ya Matamasha ya Cheka Tena(Laugh Again Concert ) Tar 4 March 2012,Pale Landmark Hotel,Ubungo,Dsm.


Crown Chavala
Baada ya mafanikio makubwa ya uzinduzi wa matamasha ya Cheka Tena mwishoni mwa mwaka jana, Nov 20 2011 pale Crystall hall ya Blue pearl hotel, Ubungo plaza. Sasa mbeba maono wa Matamasha hayo Mtumishi Freddy Chavala ameamua kuanza rasmi MSIMU WA KWANZA(SEASON ONE) wa matamasha hayo ya stand up comedy Tanzania, na Tamasha la kwanza la LAUGH AGAIN CONCERT mwaka huu litakalofanyika pale Ibungira hall katika ukumbi wa  LANDMARK HOTEL Ubungo river side, jumapili ya kwanza ya march(4th March 2012), kuanzia saa nane na nusu mpaka mbili usiku(2:30pm-8pm). 

Mbali na CROWN CHAVALA,Tamasha hili la Ubungo litawapandisha comedians chipukizi watano ambao ni Senior ABBY, Gerald Mrema, Richard Chidundo, Josephine Lukweto na MC MANU a.k.a Pilipili ya Sherehe toka Dodoma,Makundi mengine ya watu watakaonogesha tamasha hili ni pamoja na kundi maarufu la vijana waimbaji waitwao GLORIOUS CELEBRATION BAND, pia DAR ES SALAAM GOSPEL BAND, VOCAPELLA GROUP, VICTOR ARON,MADAM RUTH &CHRISS na wengine wengi bila kusahau kundi la DANCE.

Glorious Celebration watakuwepo Landmark Hotel wakimsindikiza Chavala
LAUGH AGAIN CONCERT One One litahusisha Stand Up Comedy(Zaidi), pamoja na Acapella, Dance,Sebene,Story telling, Zawadi & Suprises, Open Mic,Drama,na mengine mengi yatokanayo! Mbali na hayo kutakuwa na uzinduzi wa FORUM iitwayo QUALITY-LOVE.com, ambayo itakuwa maalumu kwa ajili ya kujadili maswala ya Upendo safi kwa kina,ubora,upana na ubora wake katika nyanja mbalimbali za maisha ya binadamu. Na kama mambo yataenda kama yalivyopangwa kutazinduliwa kitabu kiitwacho “NO MORE SCHOOL FOR YOU”(Your birth was your Graduation) By FREDY E. CHAVALA.

Kiingilio kwa tamasha hili itakuwa 5000/= kwa tiketi, ambazo zinapatikana Victory Christian Centre(VCC);Tarakea Restaurant(Mwenge),Silver Spoon and Tausi Fashion pale Mlimani City,Global Publisher na Praise Power Radio
Lakini pia mtu anaweza kununua tiketi kwa M-Pesa (0753 883 797) au Tigo Pesa (0713 883797) kwa kutuma 6000/= na atapata tiketi yake mlangoni, lakini hakikisha unatuma pesa kwa namba yako mwenyewe iliyosajiliwa kwa jina lako!

LAUGH AGAIN CONCERT Season One itakuwa na matamasha nane katika mikoa mitano ya hapa nchini kwa kuanzia, Matamasha haya yatafanyika kuanzia March-August/September 2012 katika mikoa ya Dar es salaam(3),Arusha(1),Mwanza(1),Dodoma(2) na Mbeya(1).
Tar 1st April ni ARUSHA 
29th April ni ndani ya COLD CREST HOTEL,Mwanza 
then DSM tena !



 By Crown Chavala,The King of Standup Comedy! Alimaarufu kama President Chavala!