Home

Thursday, February 23, 2012

Wakristo nchini China wafurahia Mafanikio ya Jeremy Lin


Jeremy Lin kushoto akishoot
Jeremy Lin's ni Raia wa China ambaye kwa sasa yuko nchini Marekani akicheza mpira wa kikapu katika ligi ngumu na maarufu ya mchezo huo iitwayo NBA. Jeremy ameokoka na ame-make headlines kwenye vyombo vingi vya habari nchini Marekani hasa kwa uwezo wake wapo uwanjani, kwa sasa Jeremy anaichezea timu ya New York Knicks.

Wachina wengi wanafurahia mafanikio ya Jeremy kwa kuwa anaitangaza nchi yao,lakini kwa upande wa pili Wakristo walioko nchini China wao wanafurahi mara mbili kwanza wanaona kufanya vizuri kwa Jeremy ni kumtangaza Kristo nchini humo kwa kuwa ukristo umekuwa ukipigwa vita kwa hali ya juu, na pili anaizangaza nchi hiyo.

Jeremy Lin's kipindi akiichezea timu yake ya Chuo
Jeremy kabla hajaingia NBA alikuwa akisoma katika chuo kikuu cha Havard na kuchezea timu ya kikapu ya chuo hicho iitwayo Harvard's basketball team kisha akajiunga na Houston Rockets.Akiwa chuoni hapo alikuwa akiongoza Bible study katika group la watu 80.Hadi kufikia wiki hii Kwa takribani michezo sita mfululizo Jeremy ameweza kuifungia timu yake wastani wa poits 20 kwa kila mchezo kitendo ambacho kinadhihirisha ufanisi wa Mtumishi huyu.

Ndani ya jamii ya wachina wao, hawaamini katika dini, na wengi wa wakristo hususani waliookoka wanakazi kubwa ya kuwaelimisha wenzao ambao dhana ya upagani Imetawala katika fahamu za wachina wengi.kitendo cha Jeremy kukiri wazi kuwa YESU ndiye anayemuwezesha kufikia hapo alipo kwa kiasi kikubwa imeshitua fahamu za wachina juu ya ukristo.

Wiki iliyopita hiki kitu kilimkuta Masihi wa Bwana Jeremy
Alipokuwa akitoa ushuhuda wa maisha yake katika kanisa la River of Life Christian Church lililoko Calif Santa Clara, Jeremy alisema "Everything in my life are blessings from God, I look back and I realize these are His fingerprints all over my story," Lin said, adding that "our true prize ... was something in heaven, not on earth.""I realize I had to learn ... to stop chasing the perishable prizes of this earth ... and give my best effort unto God and trust Him with the results." 

Angalia Mtupo wa mbali(long Shoot) kutoka kwa Jeremy katika moja ya Mechi za timu yake ya New York Knicks

1 comment:

  1. whaaat!!?didnt know the guy is saved!!ni mkali ile mbaya katika hay mambo yetu haya.......got an extra reason to be a fan!

    ReplyDelete