Home

Wednesday, March 7, 2012

Andrew Mwesigwa Afurahia Ushindi

Andrew Mwesigwa akiwa amebeba kombe baada ya kukabidhiwa
Andrew Mwesigwa sio jina geni kwa kanisa la uganda,kwa kuwa kwa nchini humo amekuwa ni mchezaji wa kwanza wa mpira wa miguu aliyeokoka na kufanikiwa kuwa Captain wa Timu ya Taifa ya Uganda(Uganda The Cranes).Kwa sasa Andrew Mwesigwa pamoja na Familia yake  wanaishi nchini kazkhstan kama international Player katika timu ya Fc Ordabasy.
Jana timu yake Hiyo ilifanikiwa kuchukua Ubingwa wa ligi kuu ya nchi hiyo na hiyo ni moja kati mafanikio ya mwana Afrika Mashariki  huyu.Baada ya kukabidhiwa kombe hilo(Trophy) Mwesigwa alipata bahati ya kushikana  mkono na Rais wa nchi hiyo.Mwaka juzi mwishoni (2010) wakati wa mashindano ya  kombe la CHALENGE yaliyofanyika uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam na yeye akiwa Captain, aliiwezesha The Cranes kushika nafasi ya Pili katika michuano hiyo.
Baada ya kuchukua ushindi wa pili na kufika jijini Kampala walipata Zawadi nyingi ikiwemo Kampuni ya bia nchini humo kuwapa kila mmoja Creti la Bia  kitendo ambacho Mwesigwa aligoma kulichukua na hivyo kuwaachia. 
Mwesigwa na Mkewe na mtoto wao wakiwa na spiritual family yao iliyowapokea na kushirikiana nao katika utumishi alipokua akisheza nchini Iceland
Kwa Tanzania kiukweli kama Hosanna Inc imekuwa ikitafuta japo mchezaji wa Ligi kuu ya Vodacom hapa nchini aliyeokoka ili kufanya naye interview ili kujua changamoto za utumishi wake, na anapush vipi KingDom katika Carieer yake, lakini na bado hajapatikana na uchunguzi unaendelea.

No comments:

Post a Comment