Home

Sunday, March 25, 2012

Flora Mbasha na Mumewe watembelea Ubalozi wa Marekani na Idhaa ya habari ya Voice of America(VOA)


Flora Mbasha na Mumewe wakihudumu nchini Marekani

Wakati imeonekana kama ni kawaida kwa wanamuziki wa nyimbo za Duniani kwenda na kufanya matamasha katika bara la ulaya na America, hivi karibuni wanamuziki wa injili kutoka Tanzania Flora Mbasha na Mumewe Emmanuel Mbasha wamekuwa nchini Marekani wakimtumikia Mungu kwa njia ya uimbaji.Ziara hiyo iliyoanza takribani wiki moja iliyopita ambapo ijumaa iliyopita kwa pamoja waliweza kutembelea Makao makuu ya kituo cha habari  cha  Voice of America(VOA) yaliyoko Woshington DC.

Pamoja na kutembelea idhaa hiyo, watumishi hao walipata mualiko wa kutembelea ofisi za Ubalozi wa Tanzania nchini Marekani mualiko ambao ulitoka katika kwa Balozi wa Tanzania nchini humo mama Mwanaidi Maajar.

Flora Mbasha na Mumewe wakiwa Makao makuu ya Voice of America (VOA)

Flora Mbasha akiwa na Khadija Riyami mmoja wa watangazaji mashuhuri wa VOA

Flora Mbasha akiwa katika studio za VOA pamoja na Producer Dwayne na sound Engeneer Shedrack

Flora Mbasha akiwa na Balozi wa Tanzania nchini Marekani mama Mwanaidi Maajar

Flora Mbasha na Mumewe Emmanuel Mbasha wakiwa mbele ya ubalozi wa Tanzania nchini Marekani

Hosea akasema Mungu ataturudishia miaka ile iliyoliwa na Ntununtu, Madumadu, Parale...



 Wakati watumishi hao wakifanya ziara ya kumtumikia Mungu nchini Marekani, mwaka jana mwishoni  waimbaji wengine wa injili nchini Upendo  Nkone,Upendo Kilahiro na Christina shuho kwa pamoja walikuwa nchini Marekani wakimtumikia Mungu.


Upendo  Nkone,Upendo Kilahiro na Christina shuho walipokuwa nchini Marekani mwaka jana

No comments:

Post a Comment