Home

Thursday, March 29, 2012

Manny Pacquiao asema Mungu amesema naye kwenye ndoto na Kumwambia aachane na ndondi


Manny Pacquiao akiwa na moja kati ya mikanda ya ubingwa aliyowahi kuitwaa

Kwa baadhi ya watu Jina Manny Pacquiao(33) linaweza kuwa geni masikioni mwao,Mheshimiwa Manny Pacquiao ni raia wa nchi ya Ufilipino na ni mbunge  wa bunge la nchi hiyo.Ulimwenguni kote Manny Pacquiao amekuwa maarufu sio tu kwa sababu ni Mbunge nchini mwake bali ni uwezo wake wa kurusha makonde mazito na ufundi wa hali ya juu wa kukwepa makonde.Manny pacquiao licha ya ubunge amefanikiwa kuchukua mikanda mingi ya mchezo wa ngumi duniani

Jummane iliyopita Manny ambaye ni mkatoriki alihudhuria Bible study  kanisani kwao kwa nia ya kujifunza Biblia .Akiwa katika Bible study aliwaambia wenzake kuwa Mungu amekuwa  akiwatumia yeye,Basketballer Jeremy  Lin pamoja na Tim Tebow  kwa kuwa anawahitaji kwenye ufalme wake.

Katika mahojiano yake siku kadhaa zilizopita na kituo cha redio cha DZMM cha nchini ufilipino,Manny alisema kuwa Mungu alimtokea kwenye ndoto na kumwambia aachane na Mchezo wa ngumi,Pacquiao akaendelea kusema na hapa namnukuu "I will not stay long in boxing because he said(GOD), 'You have done enough. You have made yourself famous but this is harmful," Pacquiao said”.

Manny Pacquiao  kushoto akiwa ulingoni

 

 


No comments:

Post a Comment