Home

Thursday, March 15, 2012

Mchungaji wa Rihana Asema Rihana anamuhitaji Yesu na sio Chriss Brown

Rihana

Aliyekuwa mchungaji wa Mwanamuziki Rihana Bishop Vibert Lowe amesema Rihana kwa sasa anamuhitaji Yesu na si Chriss Brown kama ambavyo wengi wanafikliri.Mch Lowe mwenye miaka 64 na raia wa kisiwa cha Barbados alikuwa pastor wa Rihana pamoja na familia yao wakati mwanadada huyo akiwa nchini kwao kabla hajaamua kutimkia nchini Marekani kwa shughuli zake za Muziki.

Kauli ya Mch huyo imekuja baada ya Chriss Brown na Rihana ambao miaka mitatu iliyopita walikuwa wapenzi na mwaka huu kuonekana tena pamoja. Mch Lowe akaendelea kusema tabia ya Rihana imebadilika sana kwa sasa watu wengi wanamuombea.

Pamoja na Rihana kutumia muda mwingi katika shughuli zake za muziki nchini Marekani,mara kadhaa amekuwa akirudi nchini mwake, pamoja na Rihana kuwa anarudi nchini Mwake Mch Lowe anasema "I don't see her much when she comes back -- she seems too busy -- but she should spend more time in church," 

1 comment:

  1. Rihana anahitaji maombi sana kwani ni mkono wa Yesu tu ndio unaoweza kumuokoa kutoka kwa Freemason. wanamuziki wengi. wamepotea na wanamwabudu shetani ili wawe maarufu. Na vijana bila kujua wamekua mashabiki wakubwa wa wanamuziki hao ambao kazi yao ni kuupotosha ulimwengu na kuwafanya watu wa mwasi Mungu kupitia Muziki wa kishetani. wana promoti mapenzi na uzinzi. nawaombea waimbaji na wanamuziki wamrudie Mungu wa mbinguni kwani saa ya hukumu yake inakuja

    ReplyDelete