Home

Wednesday, March 28, 2012

Nini Motive ya Kushiriki kwenye Gospel star search ?


Rebeca Malope moja kati ya matunda ya Gospel star seach nchini Afrika ya kusini

Kwa mtu anayesoma Biblia ataona kuwa kiutumishi Eliya hakumtoa Elisha(hakumfanya Elisha akubalike mbele za Mungu) isipokuwa kiu ya Elisha kutaka kumpendeza Mungu ilimfanya Mungu amuwezeshe Elisha kuvaa viatu vya Eliya.Kabla Mungu hajampa huo uwezo Elisha, Mungu  alimuandaa Elisha  kwa muda mrefu akiwa chini ya Eliya.Kwa Level aliyokuwa nayo Elisha, hata kama Eliya angeendelea kuwepo Elisha asingeutupa wokovu na Utumishi bali angedumu katika utumishi.

Ni rahisi kuamini  kuwa Eliya alikuwa ni lift kwa Elisha kiutumishi,lakini ni Lazima tuende mbali na kujua kuwa kabla Mungu hajaridhia jambo hilo alihakikisha kuwa ameshamfunda Elisha kwa viwango vya juu kiasi cha kujiridhisha kuwa Elisha anaweza kuvaa viatu vya Eliya.Ndio maana Elisha alipoichukua nafasi ya Eliya, nafasi hiyo haikumpa taabu,haikumfanya apoteze utukufu wa Mungu bali aliendelea kumtumikia Mungu kwa uaminifu.

Wiki hii tumeshuhudia kamati ya inayoandaa Gospel star seach kwa mwaka 2012 ikithibitisha kuwa mwaka huu kutaendeshwa zoezi hilo.Kurudi kwa Tanzania Gospel  Star seach  baaada ya miaka saba ya ukimya, kunaweza kutafsiriwa kuwa ni kurudi kwa tumaini katikati ya wanamuziki wa injili hususani ambao kiu yao kubwa ni kutoka(Nikimaanisha kufahamika).Kwa wanamuziki wanaochipukia ni lazima wajue suala la kutoka ni lingine na suala la kufanya makusudi ya Mungu ni lingine.

Hivyo kabla underground singer wa gospel hajachukua fomu ya kushiriki Gospel Star Seach ni lazima ajiulize nini Motive ya uamuzi huo,na hili litamsaidia kuweza kubeba gharama za uamuzi huo.Ni vizuri kwa washiriki wenye nia ya kutoka kutambua kuwa GOSPEL STARSEACH haimtoi mtu,bali kiu ya dhati ya mtu kutaka kufanya makusudi ya Mungu ili kuziponya roho za watu ndio humfanya Mungu kushuka na kumuinua mtu huyo(kumtoa).

Baadhi ya Washiriki wa Tanzania gospel Music Awards ya mwaka 2005

Toka enzi za akina Daudi Mungu hu-deal na watu walio curious kutaka kufanya makusudi ya Mungu huku ya kwao wakiyaweka kando kwanza. Watu hawa hawalali,hawapumziki,hawatulii mpaka kusudi la Mungu litimie.Na Mungu anapokuja kumuinua mtu wa aina hii uwe na uhakika kuwa wakumshuha hapo juu hayupo mpaka yeye mwenyewe avulugane tena na Mungu.

Kwa wanaochukua fomu za mashindano hayo kwa ajili ya kutoka, ni bora watambue kweli wanaweza kushika nafasi za juu na kutoka  ila posibility ya kushuka chini ni kubwa na life span yao hapo juu ni ndogo.

Wapo watumishi ambao kweli hizi starseach ziliwatoa kulingana na maagano yao na Mungu, lakini wapo ambao waliwahi kushiriki katika Mashindano hayo na kushika nafasi za juu kwa lugha ya haraka haraka tunawezasema wametoka.Ukichunguza vizuri utagundua kuwa wanawezasema wametoka lakini ukweli unabaki pale pale kuwa wamekuwa maanderground sugu.Kimungu hatuhitaji kutoka, bali tunahitaji GODS FAVOUR  ili kugusa maisha ya watu kwa utukufu wa Mungu. Ndio maana kuna wagonjwa wa ukimwi wamepona kupitia Nguvu ya Mungu iliyomo ndani ya Nyimbo ya Miliam Kakete iitwayo “Natamani Kufanana Na wewe”

Ile kiu ya kutaka kutoka miongoni mwa washiriki waTanzania  Gospel starseach ikiwa kubwa kuliko kiu ya kutaka kumtumikia Mungu,huko mbele hata mshiriki huyo akija kutoka ni lazima atakuja kuharibu mahali.Ni sawa na mchungaji anayetaka kanisa lake lijae watu, huku hatumii muda mwingi kumtafuta Mungu, kumkuta mtumishi huyu akitumia nguvu za giza sio jambo la kushangaza, kwa kuwa Motive yake haikuwa Kingdom bali recognition.

Barani Afrika kuna wanamuziki wengi wa Muziki wa injili ambao wamefahamika sana baada ya kushinda kwenye kwenye hizi starseaches au auditions.Na wanamuziki wengi wakubwa wamekuwa wakitumiwa kama majaji katika mchakato mzima wa kuwapata washindi wa Mashindano hayo.Miongoni mwa wanamuziki wa injili waliopata kujulikana sana baada ya kushinda kwenye starseaches na auditions ni pamoja na

Ucheagu(Uche Double Double)
Rebecca Malope
Nkhululi Bhebhe(Joyous-Tambira Jehova)

Ruth Lyanga kushoto, mdogo wake na muimbaji Lyanga George,Ruth ni mmoja wa walioshiriki katika  gospel star seach ya mwaka 2005 akiwa na umri mdogo sana kipindi hicho.kwa sasa ni mmoja kati ya Viongozi wa Tafes katika chuo cha Mtakatifu Augustino(SAUT)

Kushoto ni dada Aneth Kushaba aliyeshiriki Tanzania gospel starseach mwaka 2005, kwa sasa yuko mjomba Band katikati ni Nuruelly(Tumeagizwa Upendo) ni moja kati ya lulu ambazo kanisa bado linazihitaji


Ucheagu mmoja kati ya matunda ya Gospel star seach nchini Afrika ya kusini


1 comment:

  1. JESUS POWER GROUP internationalAugust 4, 2012 at 3:39 PM

    I want to test my talent too cos i know i can do better. please here are my numbers[0714577519'0785101290]

    ReplyDelete