Home

Tuesday, March 13, 2012

Td Jakes Aja Tena na Filamu Nyingine



Kampuni ya Td Jakes Interprises kwa Mara nyingine imeandaa Filamu ya Kikristo inayoitwa Woman Thou art Loosed on Seventh Day. Filamu hii ni mfululizo wa muendelezo wa ile iliyotoka hapo awali iliyoitwa Woman Thou Art Loosed.Filamu hii anatarajiwa kutoka Mnamo tarehe 13/04/2012,Kwa Mujibu wa Kampuni hiyo filamu hiyo imeandikwa kwa ushirikiano kati ya Cory Tynan na Askofu Thomas Dexter Jakes( T. D. Jakes). 

Wahusika wakuu wa Filamu hiyo ni Blair Underwood pamoja na  Sharon Leal,kwa wafuatiliaji wazuri wa Filamu hasa zinazotengenezwana Tyler Perry majina ya mastaa hao sio mageni kwa kuwa mamebobea katika Tasnia ya uigizaji.Blair Underwood amecheza katika Filamu kama nyingi zikiwemo “Madea’s Family Reunion” na  “Set It Off”.Mwanadada Sharon Leal amecheza vema kwenye “Why Did I Get Married Too?” Pamoja na muvie nyingine nyingi ikiwemo  “This Christmass”.

Baadhi ya washiriki wa Woman Thou Art Loosed!: On the 7th Day

Filamu hii imekuwa Directed na Award winning Filmaker mwanamama Neema Barnette,Katika Filamu hiyo inayoanza kwa Underwood ambaye ameigiza kama David na mwanadada Sharon kama Kali wakiishi maisha ya Furaha mpaka pale ambapo binti yao kipenzi alipotekwa kitendo ambacho kiliibua mambo mengi katika ndoa yao.Tofauti na mfululizo wa Woman Though art Losed ile ya kwanza na hii “On 7th Day”, Td Jakes amewahi toa filamu nyingine kama Not Easly Broken Pamoja na Jumping The Broom iliyotoka mwaka jana(2011) mwanzoni.

Moja kati ya vipande vilivyomo ndani ya “Jumping the Broom” ambayo ni another Td Jakes Output na Yeye mwenyewe alishiriki kama anavyoonekana

Ikumbukwe kuwa Woman Though art loosed ilianza kama Kongamano la Neno la Mungu ambayo iliwahusisha wanawake kutoka sehemu mbali mbali duniani kabla idea haija-expand na kuamua kuitengenezea Muvie. Kwa wote wanaomfahamu Td Jakes watakubaliana na Hosanna Inc kuwa Mafanikio ya Makongamao ya WOMAN THOU ART LOOSED yalipelekea kumuongezea heshima mtumishi wa Mungu Askofu Jakes.

You May View This Intro

No comments:

Post a Comment