Home

Saturday, March 17, 2012

Video Nyingi za Muziki wa Injili nchini, Hazina Ubunifu


Kwa mtu yeyote ambaye amekuwa curious kufatilia Ubora wa nyimbo Video za injili nchini anaweza kubaini kuwa maproducer pamoja na Production Houses za Video za Gospel nchini miaka nenda rudi revolution ni ndogo.Na hii ni kuanzia dressing,shoots,locations,nyimbo zinavyoanza mpaka zinapoisha kunakuwa kama kuna kuigana igana sana, unaweza sema tumesogea kwa mfumo wa Zero Grazing.Jaribu kutafuta album ya video iitwayo BAMBAM kutoka  Upendo Group miaka hiyo na angalia Video ya UTAMU WA YESU ya Rose Mhando iliyotoka mwaka Jana(2011) mwishoni utagundua kuna tofauti ndogo.


Crew ya AJM Production ikijipanga kabla ya kuanza kushoot,AJM yenye ofisi zake Maeneo ya Mbezi Beach jijini Dar es salaam, ni moja kati ya Production Houses kubwa zinazofanya vizuri nchini

Kwenye kila video album utakuta kuna nyimbo ya Asili hivyo mavazi yatakuwa ya Asili pia,worship au sebene kadhaa na location ni milimani, Porini, tukisogea sana ufukweni na shoots mbili tatu  za kanisani video imeisha.Kama tunataka ku-cross boarder  ni lazima tubadilike,Mungu amekusudia kupanua hozi za utumishi wetu hivyo tufanye video zilizo bora pasipo kuangalia gharama ili kuwafikia wengi zaidi duniani kote. Hii ni changamoto ambayo Kanisa la Tanzania hususani waimbaji tunapitia na siku moja itabaki kuwa hadithi kuwa tulikuwa na tatizo hili.

Kuna Production Houses ambazo watu waliookoka hawaendi wala hutowasikia sijui ni kwa kuogopa gharama au tunahisi ziko kimwili zaidi au la,kusikia video ya mpendwa imefanywa na Adam Juma(Visual Lab),Eryne Epidu(show Biz Define),au John Kalaghe bado ni msamiati. Christina Shusho amejaribu katika album yake hii mpya ya Nipe Macho ambapo sehemu kubwa  shoots za video album hiyo imechukuliwa na John Kalaghe na Mixing kufanywa na MBC Hotmedia.

Kwa sasa Duniani kote kwa upande wa video za nyimbo za Injili kumekuwa na mwamko sana wa kufanya LIVE Recording kama alivyofanja John Lisu kwenye Jehova yu Hai au kama wafanyavyo Joyous Celebration. Hii ni kwa kuwa LIVE Recording huonyesha ubora wa music na pia humpa mtu anayeangalia video uwezo wa kupata anointing  ile iliyotoka Madhabahuni wakati wa recording ilhali yuko nyumbani.

Hapa Nchini kuna video nyingi za Gospel zilizowahi fanywa na makampuni Mbalimbali ,Tofauti na LIVE Recording albums, Zifuatazo ni moja kati za Video ambazo zimekuwa na viwango vizuri vya ubora hususani kwa habari ya Creativity ukilinganisha na video nyingine.

Miriam Lukindo – Wewe Ni Sababu
Trinity Band – Usifiwe Yesu




No comments:

Post a Comment