Home

Thursday, April 5, 2012

GeorDavie Ministry yafungua tawi nchini Marekani


Kanisa la “Ngurumo ya Upako”(Geordavie Ministries) lililoko chini ya Nabii Geordavie,hivi karibuni limepata fursa ya kufungua kanisa lingine huko OAKLAND CA nchini Marekani. Hatua hii imekuja baada ya kanisa hilo la Tanzania kufuata sheria zote za ufunguzi wa kanisa nchini Marekani na kupewa kibali namba IRS 501 (C)

Kwa miaka kadhaa sasa Nabii Geodavie amekuwa akifungua matawi ya kanisa lake sehemu mbalimbali ndani na nje ya nchi. Kwa Wote waishio OAKLAND CA Marekani hususani watanzania, wanaweza kupata taarifa zaidi juu ya kanisa hilo kupitia anuani ya barua pepe ambayo ni usaoffice@geordavie.org  


Mtumishi wa Mungu GeorDavie akihudumu katika moja ya Mikutano yake katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha

No comments:

Post a Comment