Home

Wednesday, April 11, 2012

Joyous Celebration waendelea na Tour ya kuitagaza Royal Priesthood (Joyous 16)


Mabinti wa kundi la Joyous wakimba katika Joyous Celebration Annual Easter Festival iliyofanyika katika ukumbi wa Nelson Mandela Theatre wakati wa pasaka
Kundi maarufu la Muziki wa injili nchini Afrika ya Kusini Joyous Celebration limeendelea na ziara yake ya kuzunguka katika majiji matano nchini humo kwa lengo la Kuitangaza album yao mpya iliyopewa jina la Royal Priesthood ama Joyous 16 kama ilivyozoeleka na wengi.Ziara hii iliyopewa jina la The MTN Joyous Celebration tour, inakuja baada ya kundi hili kuizindua album hiyo mapema mwezi huu.

 The Most leading Gospel Group in Africa
 Kwa Mujibu wa mmoja wa Viongozi wa Kundi hilo Lindelani Mkhize,Joyous pamoja na kuimba kwenye majiji  hayo pia watakuwa wakifanya Road Shows pamoja na Music Workshop.Ziara hiyo ilianza rasmi jumanne ya wiki iliyopita ambapo kwa sasa kundi hilo linatarajia kufanya ziara hiyo katika majiji yaliyobaki ambayo ni Port Elizaberth, pamoja na Durbun na kiingilio kwa onyesho moja ni kati ya Randi 200 mpaka 300 ambayo ni sawa na shilingi elfu 40,314 mpaka 60,471 za Kitanzania.


No comments:

Post a Comment