Home

Wednesday, April 25, 2012

Package From Altar:Ushirika na Roho mtakatifu – Mwl Mgisa Mtebe



Huwezi kutawala mwili pasipo Roho,Roho ndiyo inatawala mwili, ulimwengu wa Roho ndiyo ulioumbwa kwanza na ulimwengu wa mwili ukafyatuliwa,kutoka ulimwengu wa Roho.

Baba anasema tufanye mtu, Mwana anakwenda kufanya mtu, ni Roho Mtakatifu anayekwenda kudhihirisha ule udongo wa tope unakuwa mwili, nyama,damu na mifupa mtu anakuwa nafsi hai. Ni baba anayesema mguse kipofu, ni Yesu anayemgusa kipofu , ni Roho mtakatifu anayerudisha golori kwenye macho ya kipofu.


Mwl Mgisa Mtebe

Rumi 8 :29
Usijilinganishe na mtu mwingine yeyote,jilinganishe na Kristo tafuta kufanana na Yesu, si sawa kabisa kujazwa na Roho Mtakatifu kisha ukawa mtu wa kawaida,
Kanuni za kawaida kabisa zikikugomea  lile gape la tarajio na uhalisia linapokuja unafanya nini, ulikuwa unatarajia hiki kikaja hiki kuna gape hapo,hapo ndipo unaingiza kitu kinaitwa gia ya Imani, unaaply the supernatural kwa kuwa NATURE imeku-dissapoint.Ulitegemea ukisoma utafaulu lakini kadri unavyoendelea kusoma matokeo yanazidi kuwa mabaya kuna gape hapo kati ya kusoma na matarajio.Sasa unalijazaje hilo gape hapo kati ya tarajio na hali halisi.Wewe umeokoka hutakiwi kuiba mitihani wala kuibia ukiwa katika chumba cha mitihani ili na baadaye uende mbinguni vile vile, usije ukapata “A”ukaenda jehanum.Palipo na gape kati ya tarajio na uhalisia ndipo gia ya imani huingia.

Kuna namna mtoto wa Mungu anaweza akaishi duniani bila kujichafua na akapingana na  changamoto zote za maisha ya kikristo na akashinda, akawa succsesfull duniani na mbinguni akaingia.Kuna kanuni zake, pale maisha yanapokuwekea gape ndipo unaingiza gia ya Imani. Kuna vitu vingi vinachangia katika uwezo wa mtu wa kiakili, kitaalamu intellingent quotient(IQ). Unataka kufaulu unataka kukumbuka, unakuta unaomba na unalala darasani kisha haufaulu, lakini wapo ambao kabla ya kwenda kusoma wanaenda vuta bangi.Matokeo yakija wao manapata A na wewe unapata ”C”  wakati na kunena kwa lugha unanena.

Tatizo la kiakili sio lazima liwe limechangiwa na mapepo, kitaalamu wataalamu wa saikolojia wanasema wakati baba yako na mama yako wanakutafuta walikuwa katika hali gani, kama walikuwa mawekasilishana, wanawaza madeni na matatizo, vile vichembechembe vinatengeneza makeup ya wewe baadaye, na hata wakati umetungwa mimba mama yako alikuwa katika hali gani, kama alikuwa mtu wa machozi,kukasirika, kulalamika hivyo vichembechembe viliingia, na alikuwa anakula chakula gani hilo nalo ni la msingi.

Na hata wakati unazaliwa ulikaa sekunde ngapi ukikosa hewa, kama ulikaa muda mrefu pasipo kuvuta hewa, uwezo wa kiakili hushuka.Hapo utaona uwezo wa kiakili hauchangiwi tu na mambo ya kiroho.Haya sasa umeshazaliwa katika mazingira hayo na uko first year unafaulu vipi? Ukijikuta katika hali hiyo ya kimasomo hapo ndipo Imani hutumika, wakati wengine wanatarajia ufeli lakini kwa imani unalijaza hilo gape na kufaulu
Unamawazo ya kuwa Lawyer, Accountant, daktari anakwambia moyo wako umechoka,au anasema una kansa ya damu,umetarajia biashara itaenda hivi inaenda hivi, maisha yanakufrastrate yanakutendea visivyo.Hapo ndipo NGUVU ya imani inapoingia kazini,kila mtu anaye kujua kiuchumi, kiakili anashangaa umefika vipi upande wa pili na umewaacha watu wote midomo wazi.

Yesu aliposema nyumba iliyojengwa juu ya mawe alimaanisha nini,yale mawe hayahitajiki siku zote yanahitajika siku ya Dhoruba na siku ya tetemeko,dhoruba isipokuja tetemeko lisipokuja aliyejenga juu ya mawe na juu ya mchanga hakuna tofauti,the only defference ni siku ya disaster.

Wakati wengine wanafaulu hali kwako inakuwa ngumu, usione kuwa kuendelea kusali ni kitu kama mzigo vile, wee endelea kuwekeza kwa kuwa kuna siku ya dhoruba.Tunajifunza haya mambo ili tuweze kupata kila kitu ambacho Mungu alitukusudia cha kutuwezesha  kuishi maisha ya ushindi na mafanikio duniani. Hatukuitwa kuteseka, hatukuitwa kushindwa, kufeli kuhangaika.Huwezi kufanikiwa katika ulimwengu huu pasipo kutumia nguvu fulani ya Kiroho.

Huwezi kutawala mwili pasipo Roho,Roho ndiyo inatawala mwili, ulimwengu wa Roho ndiyo ulioumbwa kwanza na ulimwengu wa mwili ukafyatuliwa/ ukazaliwa  kutoka ulimwengu wa Roho.Sio kwamba ulimwengu wa Roho uliumbwa kushoto ulimwengu wa mwili ukaumbwa kulia, ulimwengu wa Roho uliumbwa kwanza ulipokamilika  vilivyokuwa ndani ya ulimwengu wa Roho vikazaa ulimwengu wa mwili.

Hivyo ulimwengu wa mwili umetokea katika ulimwengu wa Roho,huwezi kutawala ulimwengu wa mwili, bila kupitia nguvu ya kiroho.Unahitaji nguvu za MUNGU,na Roho mtakatifu ndiye NGUVU YA MUNGU, ndiye anayewezesha kauli ya Baba na matendo ya mwana yanakuwa dhahiri. Baba anasema tufanye mtu, Mwana anakwenda kufanya mtu, ni Roho Mtakatifu anayekwenda kudhihirisha ule udongo wa tope unakuwa mwili nyama damu na mifupa mtu anakuwa nafsi hai. Ni baba anayesema mguse kipofu, ni Yesu anayemgusa kipofu, ni Roho mtakatifu anayerudisha golori kwenye macho ya kipofu.

Kwa kupewa Roho mtakatifu ni kukufanya uwe kama Yesu,kwa kuwa anakuambukiza uwezo aliokuwa nao Yesu.  1Yoh 4: 12-17 “Kama yeye alivyo na sisi ndivyo Tulivyo” Rum 8: 29, Efeso 4; 11-14.Mungu anataka uwe YESU Mdogo duniani, ufananishwe na mfano wa mwanawe, watu wote wanaomhitaji Yesu waje kwako kwa kuwa yeye alivyo ni kama wewe kwa kuwa umepewa Roho wake.

Itaendelea......
Mwl Mgisa Mtebe

No comments:

Post a Comment