Home

Saturday, April 14, 2012

Rais Hugo Chaves amuomba Yesu amponye Kansa ili aweze kuwatumikia wana Venezuela


Mh Hugo Chaves
Rais wa Venezuela Mh Hugo Chaves hivi karibunibaada ya kutoka nchini Cuba kwa matibabu ya Cancer, alimuomba Yesu Kristo amuokoe na Mauti ili aweze kulitumikia Taifa lake.Mh Chaves alitoa rai hiyo kupitia Television ya Taifa ya nchi hiyo.

Rais Chaves ambaye ni mkatoriki alisema na hapa ninamnukuu “Give me your crown, Jesus. Give me your cross, your thorns so that I may bleed. But give me life, because I have more to do for this country and these people. Do not take me yet,” Chávez expressed, as he stood below a statue of Jesus with the crucifix.”

Rais Chaves kwa muda sasa amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kansa ambapo mpaka sasa chanzo cha kansa hiyo hakijajulikana na ugonjwa wake huo umekuwa ukiwekwa katika hali ya usiri mkubwa huku jamii kubwa ya wanavenezuela ikiwa haijui kwa undani juu ya ugonjwa huo unaohatarisha afya ya rais huyo.

Wakati huo huo kiongozi wa upinzani nchini humo bwana Henrique Capriles ambaye anawania kiti cha Urais wan chi hiyo, amemtakia afya njema Rais Chaves na amemuombea apone mapema ingawa amekuwa akimpinga Rais Chavea kwa kusema kama Yesu Kristo angekuwepo leo asingekuwa Bepari kama alivyo Rais Chaves.

No comments:

Post a Comment