Home

Sunday, April 8, 2012

Tamasha la Pasaka 2012 limesheheni Vyote,watumishi waabudishaji(worshipers) na watumishi waliobobea kwenye kusifu(Gwaride)



Rebeka malope akiwa pamoja na waumishi wa Mungu Upendo kilahiro, Ephraim Sekeleti,Solomon Mukubwa siku ya ijumaa mara baada ya Malope kuwasili uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa JK Nyerere

Ni ukweli usiofichika kuwa katika Mwili wa kristo Mungu ameugawanya katika viungo mbalimbali hususani huduma tano ambazo ni waalimu, mitume, manabii, wachungaji, wainjilisti. Kwa Habari ya uimbaji nako Mungu ameweka uwezo wa kuimba kwa namna kubwa mbili yaani kusifu pamoja na kuabidu.

Leo tarehe 8-04-2012 katika Tamasha la Pasaka kuna waimbaji ambao ukichunguza kwa undani utagundua  wame-base upande mmoja, kuna ambao ni Worshipers na wapo ambao Mungu huwatumia sana katika kusifu, hivyo pale uwanja wa Taifa naamini Itafanyika ibada kamili ya kusifu na kuabudu.

Miongoni mwawatumishi watakaohudumu ni pamoja na Upendo Kilahiro, Solomon Mukubwa, Anastazia Mukabwa, Rebeka Malope, Rose Muhando , Christina Shusho,Upendo Nkone,Glorious Celebration na Ephraim Sekeleti kutoka Zambia.Kati ya hao hapo juu ukichunguza kwa Makini utaona wapo ambao ni watu wa Praise na wapo ambao ni watu wa Worship.

Upendo kilahiro

Anastazia Mukabwa na Rose Muhando wakati wa Tamasha la Pasaka jijini Mwanza Mwaka jana

Ephraim Sekeleti

Christina Shusho

Rose Muhando akiimba wimbo wa NIBEBE wakati wa Tamasha la  Pasaka 2011 katika Uwanja wa CCM jijini Mwanza 




No comments:

Post a Comment