Home

Wednesday, May 2, 2012

John Lisu kurekodi LIVE album yake ya pili Mwezi November


John Lisu akiwa studio wakati anarekodi album yake ya pili
Mwanamuziki mahiri wa nyimbo za Injili nchini John Lisu,mnamo tarehe 4/11/2012 anatarajia kurekodi LIVE album yake ya pili katika kanisa la City Christian Centre lililoko Upanga jijini Dar es salaam.Akiongea na Hosanna Inc mara baada ya Tamasha la kusifu na kuabudu ambalo hufanyika kila mwisho wa mwezi katika kanisa la Dar es salaam Pentecost Church, Lisu alisema yuko katika maandalizi makali ya kufanikisha zoezi hilo.

Lisu aliendelea kusema mpaka sasa amesharekodi jumla ya nyimbo tatu za audio, kati ya nyimbo hizo nyimbo yake ya "UKO JUU" ambao ndani yake ameuelezea ukuu wa Mungu tayari ameisha itoa na unaweza isikiliza hapa chini. Sambamba na hilo John Lisu katikati ya mwezi huu wa tano natarajia kwenda nchini Kenya katika jiji la Mombasa kwa ajili ya kuendeleza JEHOVA YU HAI TOUR.Lisu ni mmoja kati ya waimbaji ambao ijumaa ijayo ya tarehe 4/05/2012 watawaongoza mamia ya watu katika usiku wa kusifu na kuabudu uliopewa jina la AFLEWO(Africa Lets Worship) utakaofanyika katika kanisa la City Christian Centre.

Sikiliza nyimbo mpya ya Lisu "Uko Juu"

No comments:

Post a Comment