Home

Friday, May 11, 2012

Mshauri wa Kiroho wa Rais Obama asikitishwa na kauli ya Obama kuunga mkono ndoa ya Jinsia Moja


Rais Obama kushoto akiwa na Mch Joel Hunter katikati  anayecheka na kulia ni Joshua Dubois mkurugenzi wa Ikulu ya Marekani kwa masuala ya Imani

Mch Joel Hunter wa kanisa la Northland  lenye watu zaidi ya 15,000 ambaye kwa muda mrefu ameaminika kama ndiye mshauri wa masuala ya  Kiroho wa Rais wa Marekani  Bwn Barack Obama, amesema amesikitishwa na kauli ya Rais Obama ya kuunga mkono ndoa ya jinsia moja .Kauli ya mshauri huyo imekuja siku moja baada ya ya Rais Obama siku ya Jumatano iliyopita kupitia mahojiano katika Television ya ABC kusema haoni tatizo juu ya ndoa ya jinsia moja.

Mch Hunter amesema kabla ya Obama kwenda katika mahojiano hayo alimpigia simu Mchungaji huyo na kumweleza kile ambacho ataenda kuongea,Mch huyo na alimwambia Rais Obama kupitia simu kuwa anapingana na uamuzi ambao Rais huyo anaenda kuuchukua.Mch Hunter amesema ingawa anapingana na maamuzi ya Rais huyo lakini hawezi kuutupilia mbali urafiki na uhusiano alionao na Rais Barack Obama.

Mch amliendelea kusema moja kati ya sababu zilizompelekea Rais Obama kumpigia simu kabla hajaenda kwenye mahojiano hayo ilikuwa ni kulinda mahusiano kati yao wawili. “Haikuwa rahisi kuliongelea hili jambo kwa njia ya simu wala mimi kumkataza asilifanye” alisema Mch Hunter

Aidha wakati Rais Obama akipiga kampeni ya kuingia Ikulu 2008 alimjumuisha Mch Donnie Mcclurkin kama mmoja wa wapiga kampeni wake, lakini kutokana na msimamo wa Donnie Mcclurkin kukemea vitendo vya kishoga ilimlazimu Rais Obama kumuengua Mchungaji huyo katika orodha ya wapiga kampeni wake japokuwa alianza naye.


Angalia Pastor Donnie Mcclurkin akiongelea na kukemea Vitendo vya Kishoga kwenye Mkutano wa kampeni za OBAMA mwaka 2008



No comments:

Post a Comment