Home

Tuesday, May 22, 2012

Somo Kutoka kwa Mwl Mwakasege - Ikimbieni Zinaa 2



“Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwako nyakati za hatari. Maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe, wenye kupenda fedha, wenye kujisifu, wenye kiburi, wenye kutukana, wasiotii wazazi wao, wasio na shukrani, wasio safi…….Kwa maana katika hao wamo wale WAJIINGIZAYO KATIKA NYUMBA ZA WATU, NA KUCHUKUA MATEKA WANAWAKE WAJINGA WENYE MIZIGO YA DHAMBI, waliochukuliwa na tamaa za namna nyingi. (2 Timotheo 3:1,26).

Mwl Christopher Mwakasege
Je! Siku hizi wanawake hawatekwi mateka na wanaume ili wafanye mambo ya zinaa? Vishawishi vimekuwa vingi, na wanawake wengi wameanguka katika mitego hiyo ya kupenda fedha na anasa, na mwisho wake ni kufanya uzinifu.
Kwa nini wanaume wengi wamekosa akili juu ya jambo hili. Ni kitu gani kimewapofusha macho wasione ya kuwa uzinifu ni mbaya? Biblia inasema; “Mtu aziniye na mwanamke hana akili kabisa; afanya jambo litakalomangamiza nafsi yake.” (Mithali 6:32)

Ni dhahiri ya kwamba palipo na zinaa pana uharibufu, na wengi wanaangamia. Na nataka nikuambie ya kuwa Roho Mtakatifu akikuwekea mzigo huo ndani yako na kuliona jambo hili jinsi linavyomhunish Mungu, hakika hutatulia; na hapana budi macho yako yatajaa machozi juu ya kizazi hiki kinachojiangamiza chenyewe kwa sababu ya zinaa.

Sababu ya mambo haya kuandikwa.
Mambo haya hayakuandikwa kwa bahati mbaya, wala si kwa ajili ya kuonyesha historia ya watu Fulani tu. Bali yaliandikwa kwa kusudi maalumu na muhimu.
“Basi mambo hayo yaliwapata wao kwa jinsi ya mifano, yakaandikwa ili KUTUONYA SISI, tuliofikiriwa na miisho ya zamnai – Kwa hiyo anayejidhania kuwa amesimama na aangalie asianguke.” (1 Wakorintho 10:11,12)


Na mimi nimependa kuyaonyesha wazi ili tujue tunapozungumza juu ya zinaa, Bwana Mungu anakuwa na mawazo gani juu yake. Nafahamu si mara kwa mara hata katika mahubiri na mafundisho, jambo hili huguswa kwa undani. Lakini naona umefika muda wa kulichambua jambo hili kwa undani zaidi.

Hali ilivyo sasa.
Mtu mmoja aliniuliza “Je, mtu aliyeokoka anaweza kufanya mambo ya uasherati – je, anaweza kuzini?”
Nikamwambia, “Mtu aliyeokoka hatakiwi kufanya mambo ya uasherati, kwa kuwa kufanya hivyo ni dhambi, lakini asiposimama katika Kristo sawasawa anaweza kuzini.”

Halafu huyo mtu akaendelea kuuliza, “Je, Unamfahamu Fulani? (Akamtaja jina lake).
“Ndiyo namfahamu.” Mimi nilimjibu, na nikaendelea kusema; - “ kuwa ni mtumishi wa Mungu, ingawa sijamwona muda mrefu umepita sasa”.
Ndipo akasema, “Unafahamu ya kuwa alianguka na akazini na msichana Fulani (akamtaja jina lake) ambaye pia ameokoka, na sasa yule msichana amezaa?”
Mimi nilishangaa na kushutushwa na habari hizo. Nikamuuliza “Unasema kweli ndivyo ilivyotokea?”
Akasema, “Ndiyo”

Ndipo Roho wa Mungu aliponikumbusha ndoto ile aliyonipa. Katika ujumbe ule wa ndoto, Mungu alinionyesha mkristo aliyeokoka akifanya mambo ya uasherati.
Kwa mtu asiyeokoka siwezi kushangaa akifanya uzinzi, kwa kuwa bado yuko gizani, na yuko chini ya mkuu wa giza, ibilisi – kwa hiyo anaweza kufanya lo lote lile. Ndiyo maana mtu anaweza kusema yeye ni mkristo, na huku anazini mara kwa mara.
Mkristo wa kweli aliyeokoka hatakiwi kuzini, wala kushindwa na dhambi. Kwa nini? Kwa kuwa ndani yake ametengwa mbali na dhambi, na amepewa ushindi juu ya dhambi.


Na Mwl C.Mwakasege 

8 comments:

  1. Hongera Mwl.Mwakasege, somo hili limekuja kwa wakati mwafaka sana,hiki nikipindi ambacho watu wake kwa waume wametawaliwa na tamaaza mwili.Hakika insikitisha sana kuona wanawake wanauza miili yao hadharani kama bidhaa , na wanaume wanaenda kuchagua bila iabu na baadhi yao wapo kwenye ndoa, mbaya zaidi baadhi yao uatawakuta kanisani wakijitangaza wameokoka.

    Aidha ni muda sasa umefika sasa uasherati na madhara yake kuhubibiriwa na kukomewa makanisani bila aibu maana jamiii inaangamia.

    ReplyDelete
  2. Ubarikiwe mwl mwakasege huwa nabarikiwa sana na mafundisho yako. Mungu azidi kukutumia kwa ajili ya kazi. Nawatia watu wa mungu wasimkosee mungu kwa ajili ya tamaa ya mwili na tuendelee kuomba msaada wa mungu atusimamie.

    ReplyDelete
  3. Ubarikiwe Mwl. Mwakasege kwa somo zuri Mungu azidi kukufunulia ili nasi tupate kupona.

    ReplyDelete
  4. Bwana azidi kukupa mafunuo maana umekuwa msaada sana kwangu ni
    mepata maarifa sana katika masomo yako mbali mbali ninayofuatialia mitandaoni na sehemu zingine, Bwana azidi kuku ongezea muda wa kuishi.

    ReplyDelete
  5. Sifa kwa Bwana. Aliye na sikio asikie, aliye na macho ya kuona na aone akasome na afahamu.

    ReplyDelete
  6. nashukuru kwa somo hili limetupa ufahamu

    ReplyDelete
  7. Asante mtumishi wa Mungu kwa mafundisho haya, Ubarikiwe sana na Bwana, Amen.

    ReplyDelete