Home

Saturday, May 12, 2012

Viongozi wa Makanisa nchini Zimbabwe wavutana kuhusu ujio wa TB Joshua nchini humo

Nabii Tb Joshua

Viongozi wa umoja wa makanisa nchini Zimbabwe siku ya jana, umekana kumualika Nabii Tb Joshua nchini humo katika siku maalumu ya kuliombea taifa hilo (Zimbabwe National Day Of Prayers) iliyopangwa kufanyika tarehe 25.05.2012.Viongozi hao wamesema kwa kuwa siku hiyo ni ya wanazimbabwe, hivyo wao watakuwa wakifanya maombi na sio mtu kutoka nje ya Zimbabwe.

Hatua ya wachungaji na viongozi hao kusema hivyo imekuja wakati wakisambaza vipeperushi vinavyohimiza watu kujitokeza katika siku hiyo, wakati wakifanya hivyo walikumbana na maswali mengi juu ya uvumi wa kuwepo kwa Tb Joshua katika siku hiyo.Mpaka sasa inasadikika kuwa mpinzani mkuu wa Rais wa Zimbabwe Bwn Morgan Tsvangirai pamoja na baadhi ya wachungaji ndio wamemualika mtumishi huyo wa Mungu kufika nchini humo siku hiyo.

Kwa upande wa watumishi walioandaa ujio wa Tb Joshua nchini humo, wanahofia ujio huo ukazuiliwa na chama Tawala cha ZANU PF kikiamini kuwa ujio huo utakisafisha chama cha Tsvangirai(MDC). kwa upande wa waandaaji wa siku hiyo ya maombi wao wanasema kama Tb Joshua anakuja, basi waliomleta watafute jina lingine la kuiita shuhuli(Event) yao na sio nao waiite “Zimbabwe National Day of Prayers” bali watafute jina lao. 

Mmoja wa wachungaji wanaoandaa siku hiyo ya maombi alisema hao wanaomleta Tb Joshua na kufanya tukio lingine sambamba na hili walioandaa wao ni kuleta mgawanyiko kwa waumini nchini humo.

No comments:

Post a Comment