Home

Thursday, June 7, 2012

Baada ya Pretoria, Joyous Celebration kuendeleza Tour Sun City

Joyous Celebration
Kundi maarufu la muziki wa Injili kutoka nchini Afrika ya Kusini Joyous Celebration, mnamo Tarehe 30 June 2012 litakuwa likifanya ziara katika mji wa Sun City nchini humo. kundi hilo linadhaminiwa na kampuni ya simu za mikononi ya MTN, akiongea na waandishi wa habari siku mbili zilizopita nchini Afrika ya kusini, mmoja wa viongozi wa kundi hilo Jabu Hlongwane amesema mashabiki wa kundi hilo watakuwa na muda mzuri wa kumsifu Mungu wakati wa ziara hiyo. Jabu aliweka wazi kuwa pasipo Udhamini wa MTN ingewawia ngumu kufanikisha ziara hiyo

Baada ya kumaliza Sun City, Kundi hilo linatarajia kufanya ziara nyingine kubwa katika miji ya Port Elizabeth na Durban. Kwa sasa album yao ya Joyous Celebration 16(JC 16) imeripotiwa kushika nafasi ya nne kati ya hamsini kwa Album za gospel zilizouzwa sana nchini Afrika ya kusini.
 
Angalia hapa chini moja kati ya nyimbo kali zilizomo kwenye Joyous 16

No comments:

Post a Comment