Home

Sunday, June 10, 2012

Yaliyomo kwenye magazeti ya Kikristo kwa ufupi


 Gazeti la

Mwanamke Tanga alala na Jogoo kwa Miaka Miwili
Wanakijiji wa kijiji cha Msisi wilayani Handeni mkoani Tanga wameshangazwa na tukio la mama mmoja ambaye amekuwa akilala na Jogoo kwa miaka miwili huku akiteseka.Hatua hiyo imetokea baada ya mama huyo mwenye watoto sita kuchoshwa na Zoezi la jogoo huyo kila kukicha na hivyo kumpeleka mbele za watu ili aweze kuondokana na usumbufu.

Jibu la Maisha lilikuwepo wakati wa zoezi la utiwaji kiberiti wa jogoo hilo.Gazeti la jibu la Maisha lilishuhudia mama huyo akitokwa na machozi wakati wa zoezi la uchomaji moto wa jogoo hilo.Mama huyo alisema chanzo cha yote ni pale alipokuwa akifanya kila kitu na hakuona kufanikiwa ndipo alipoamua kwenda kwa mganga.Baada ya kufika kwa mganga aliambiwa na mganga huyo amlete jogoo, alipomleta mganga alimchinja jogoo huyo na kutoa moyo,alikaukata vipande na kuuchanganya na damu kisha akamwambia mama huyo ale naye akala.

Mganga huyo alimwambia arudi mara ya pili akiwa na Jogoo mmoja na mtetea,aliporudi  akamwambia asithubutu kula yai wala kuchinja kuku yeyote wa mtetea huyo.Baada ya siku kadhaa mtetea huyo alitotoa vifaranga akiwemo jogoo, usumbufu ulianza baada ya Jogoo huyo kukua, kila alipokuwa akilala jogoo huyo alimwijia ndotoni na kufanya naye tendo la ndoa akiwa mfano wa binadamu.Zoezi hilo lilifanyika kwa muda ndipo alipomrudia mganga huyo na kumuuliza kulikoni.Mganga alimjibu kuwa huo ndio ulinzi wake na hao ndio watajibu shida zake.Cha kusikitisha mateso na shida zilibaki pale pale.

Mama huyo aliendelea kuteseka kwa muda mrefu mpaka siku aliposikia kuna MKUTANO WA INJILI na wanatangaza wenye mateso na waliofungwa na shida mbalimbali watawekwa huru.Alipofika kwenye mkutano huo uliokuwa umeandaliwa na huduma ya Voice of Hope(VOH), aliombewa na kuambiwa amlete jogoo.Kwa ushirikianao na wanakijiji cha Msisi alimleta jogoo huyo kisha jogoo akachomwa moto hali iliyopelekea kukomesha mateso ya mama huyo.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alipigia Kanisa Magoti
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mh Said Mecky Sadik ameomba ushirikiano wa hali ya juu kutoka katika madhehebu mbalimbali ili kutuliza hali ya mambo katika jiji hilo lenye shughuli nyingi nchini na kitovu cha uovu.Mkuu huyo wa mkoa alitoa ombi hilo katika kikao cha pamoja na wajumbe wa kamati ya ushauri wa mkoa wa Dar es Salaam(RCC) kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano katika ofisi yake mwanzoni mwa wiki iliyopita.

Alisema suala la kuliweka jiji katika hali ya usalama litafanikiwa ikiwa taasisi mbalimbali ikiwemo makanisa na misikiti na taasisi binafsi na zile za serikali na madhehebu mengine zitashiriki kikamilifu katika zoezi hili, alisema mwakilishi huyo wa Rais.

Jumbe za uchomaji moto makanisa zaenea Dar es salaam
Watu wasiofahamika wamekuwa wakieneza jumbe kwa njia ya simu za mikononi(sms) kuwataka watu waombe kwa kuwa kuna vijana wapatao 300 kutoka kundi la uamsho la mihadhara kutoka  Zanzibar(JUWAKATA) wamesambazwa jijini Dar es salaam na Arusha kwa ajili ya kuchoma Makanisa.

Gazeti la jibu la Maisha ni miongoni wa waliopokea jumbe hizo na uchunguzi umeonyesha waliotuma ni watu wengi wakiwemo wachungaji.Uchunguzi wa gazeti la jibu la maisha umeonyesha baadhi ya jumbe hizo zinatokea Zanzibar.


Gazeti la Nyakati
Gazeti huru la Kikristo la kila wiki

Usajili wa Makanisa wawaumiza vichwa wachungaji
Wakati utaratibu wa kusajili vyama vya kijamii ikiwemo makanisa umewekewa muda wa siku tano  hadi kumi na nne kukamilisha usajili, imebainika kuwa makanisa yamewasilisha maombi zaidi ya miaka kumi iliyopita lakini bado hayajashughulikiwa huku wizara ya mambo ya ndani ikisema kuwa kuchelewa huko kunatokana na maombi hayo kufuatiliwa na vyombo tofauti tofauti vya serikali ili kujiridhisha.

Ingawa serikali imekuwa haiwabani sana watumishi wa Mungu wanaoendesha huduma zao pasipo kusajili, lakini uendeshaji wao umekuwa ukikabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo kukosa kutambulikana rasmi na mamlaka ya serikali katika maeneo yanayoendesha huduma hizo

Siri Tano Zinazowasumbua Wachungaji
Kwa desturi zao watumishi wa Mungu hususani wachungaji ni watu wanaotunza siri kwa viwango vya juu.Wanakaa na kusikiliza siri na matatizo ya watu bila kuyavujisha.Wachungaji nao wana siri zao amabazo nao huishia kuzibana mioyoni mwao.Watumishi wa Mungu wao huogopa kutoa siri zao kwa kuamini kuwa zinaweza kubomoa hudumaMwandishi maalumu wa gazeti la Nyakati yeye alipata fursa ya kuongea na wachungaji na wao wakatoa mambo yanayowasumbua 

1.Ndoa yangu ni ngumu
Kwa kuwa wachungaji kila kukicha wamekuwa wakiitwa na washirika wao ili kutatua matatizo mbalimbali kiasi cha wao kutopata nafasi ya kukaa na familia zao.Kutokana na hayo wake zao wamekuwa wakijiuliza kama waume wao wamewaoa wao au wameoa Kanisa.

2.Nahofia watoto wangu wakikuwa watalichukia kanisa
Watoto wa wachungaji  mara nyingi huambiwa mambo mabaya kuhusu kanisa,baba zao ambao ni wachungaji huofia sana endapo watoto wao watakua wakiwa na dhana hiyo vichwani.

3.Nawapa Uhuru wakosoaji wanishambulie  watakavyo
Huwa nawaruhusu sana watu wanaonikosoa kufanya hivyo kwa kuwa, kwa kuwa kama nitakuwa nikiwapinga na kuwaonyesha kiburi wanaweza kuniharibia huduma na familia yangu  
4.Mara nyingi huwa nawachukia washirika wenye uwezo wa kuwazuia wanaonihambulia lakini hawafanyi hivyo

5. Mara nyingi nimekuwa nikiwaza kuachana na huduma
Wachungaji kama waitwavyo leo ni kweli wanapenda washirika wao na huduma zao,wengi wao wamekuwa wakibeba shutuma na lawama zinazoligusa kanisa.Katika hili hupata mawazo ya kuachana na huduma.

No comments:

Post a Comment