Home

Thursday, July 12, 2012

Coctail ThankGiving Night ya Uncle Jimmy Temu Kurindima Tamaal Hotel


Jimmy akiwa Redion
Waswahili walitangulia na Kusema UJANA MAJI YA MOTO na ni Ki-Mungu kumtumikia Mungu siku za UJANA kabla hazijafika siku utakazokuja kusema kuwa siwezi.Man of GOD James Temu ni kijana na  Mtangazaji wa kituo cha Redio cha Kikristo Kiitwacho Praise Power cha JIJINI Dar es Salaam, pia Jimmy  ni Mcheza Filamu maarufu nchini na on top of it  Uncle Jimmy kama ajulikanavyo na wengi ni mmoja kati ya ma-blogger mahiri wa habari za wa Kikristo nchini Tanzania.

Mwaka jana mwezi wa saba James Temu alianzisha blog yake iitwayo www.unclejimmytemu.blogspot.com na mwaka huu anatimiza mwaka mmoja katika kuielimisha jamii kwa habari ya ufalme wa Mungu kupitia mtandao.Hivyo basi kwa kuliona hilo gentleman huyu mrefu mweupe mwenye sauti nyembamba ameamua kuwaalika wadau wote kwenye Coctail Party maalumu ya kumshukuru Mungu kwa kumuwezesha kutimiza mwaka mmoja.

Jimmy akiwa katika harakati za kucheza Filamu pamoja na Ray na Waridi
Shughuli nzima itafanyikia tarehe 20.07.2012 katika Tamaal Hotel iliyoko maeneo ya Mwenge nyuma ya kituo cha Polisi, katika usiku huo marafiki ndugu na jamaa watapata nafasi ya kumfahamu Jimmy alikotoka alipo na mataraji yake  ya hapo baadaye.Muda ni kuanzia saa 1:00 usiku mpaka 3:00 usiku kiingilio ni BURE.Kama uko Dar es Salaam hii si ya kukosa fika Tamaal na tuseme EBENEZER pamoja na mwanahabari huyu.

Sambamba na Kumfahamu Jimmy,kwa kila atakayefika atapata nafasi ya kumtukuza Mungu LIVE pamoja na Live Band kutoka kwa Dar es Salaam Gospel Band pamoja na wanamuziki wengine maarufu nchini.Katika usiku huo chakula kitatolewa bure kwa kila atakayefika ambapo watangazaji wengi maarufu nchini watakuwepo katika kumshukuru Mungu pamoja na mwanahabari mwenzao.Kwa ROHO SAFI tukutane pale Tamaal Hotel ijumaa ya wiki ijayo(20.07.2012) tuseme EBENEZER pamoja na James Temu.

Jimmy akiwa ndani ya Friends on Friday White Party ambapo ni mmoja kati ya waandaaji wake

No comments:

Post a Comment