Home

Tuesday, July 31, 2012

Love Tanzania Festival kuyakutanisha zaidi ya Makanisa 800 nchini



Miwani 10,000 za kusomea kugawiwa Bure
Wafanyabiashara wakubwa na viongozi wa serikari kuinjilishwa kupitia Evening Dinner
Kikundi maalumu cha Michezo ya Baiskeli kuonyesha ufundi wa kuchezea baiskeli
Tofauti na Donnie Moen, Nicole C Mullen  ,Christina  Shusho,John Lissu,Pastor Safari Paul wa DPC kuongoza Love Tanzania Festival Praise Team

Love Tanzania Festival ni kusanyiko kubwa la kihistoria litakalofanyika kuanzia tarehe 11-12/08/2012 katika viwanja vya Jangwani kuanzia saa saba mchana mpaka saa 2 Usiku.Kwa mujibu wa mmoja wa waandaaji wa kusanyiko hilo Brother Prosper Mwakitalima ameiambia Hosanna Inc kuwa katika kufanikisha kusanyiko hilo makanisa zaidi ya 800 yameshiriki katika maandalizi ya tukio hilo maalumu lenye lengo la kuwakutanisha watu wa dini,kabila,rika zote kwa lengo la kumtukuza Kristo Yesu.

Kwa mujibu wa Mwakitalima kabla ya shughuli ya tarehe 11 na 12 kuna shughuli mbalimbali ambazo Love Tanzania Festival itakuwa ikizifanya kwa jamii ya Tanzania.

Ifuatayo ni Ratiba ya shughuli nzima za LOVE TANZANIA FESTIVAL.

Tarehe 5 August  7:00Asbh – 10.00 Asbh
Mbeba maono wa Love Tanzania Featival  mtumishi Andrew Palau atahubiri ibada zote mbili katika kanisa la Upanga City Christian Centre (UCC)

Muimbaji mashuhuri Nicole C Mullen atahudumu

Tarehe 7 August 10Asbh
Kutafanyika Mkutano wa waandishi wa habari(Press Confference) katika Ukumbi wa TBD ambapo Andrew Palau akiambatana na wachungaji, Maaskofu,waimbaji na kikundi cha waonyesha michezo ya Baiskeli watakuwa wakiongea na waandishi wa habari.
Usiku huo wa Tarehe 7 kuanzia saa 11.30 jioni katika ukumbi wa KARIMJEE  kutafanyika WOMENS DINNER ambapo kamati imewakaribisha zaidi ya wamama 600 nao watapata nafasi kusikiliza na ya kubadilishana mawazo na Andrew Palau.

Tarehe 8 August  12:00 jioni
Katika Ukumbi wa Karimjee Hall kutafanyika hafla ya chakula cha jioni ambapo viongozi mbalimbali wa serikali na wafanyabiashara wakubwa watapata nafasi ya kukutana na Palau ambapo mtumishi huyo atatumia nafasi hiyo kumtangaza kristo kwa tabaka hilo la watanzania ambao kwa namna moja au nyingine limekuwa ni vigumu kufikiwa na injili ya Yesu kristo.

Tarehe 10:August 8:00 Mchana – 9:00 Jioni
Kutafanyika maozoezi(Rehesal)ya michezo ya Baiskeli ambapo kikundi cha JUNGLE RUSH FMX  kutoka Afrika ya Kusini kitakuwa kikifanya mazoezi hayo ili kujiweka sawa.Baada ya mazoezi hayo kutafanyika MAOMBI rasmi kwa ajili ya kuuweka wakfu uwanja wa Jangwani kwa ajili ya shughuli nzima ya tarehe 11-12.



VITUO MAALUMU KWA AJILI YA CLINIC YA MACHO
Love Tanzania Festival siyo tu itahusisha kuponya ROHO za watu kupitia neno la Mungu, pia watakuwepo Madaktari maalumu wa macho kutoka Marekani na watashirikiana na madaktari wa ki-Tanzania ambapo watakuwa wakipima watu mbalimbali wenye matatizo ya macho BURE, wale wenye matatizo ya kutoona vizuri maandishi watapewa MIWANI za kusomea BURE.Jumla ya miwani zipatazo elfu kumi(10,000) zipo kwa ajili ya kugawiwa kwa watanzania ambao watabainika na matatizo hayo, Ratiba ya Clinic hiyo itakayokuwa na vituo vinne ni kama ifuatavyo.

Kituo 1:St Nicholaus Anglican Church –ILALA
Kituo cha 2:Tanzania Assemblies of GOD (TAG-Mbagala)
Kituo cha 3:Lutheran Chuch – Vingunguti
Kituo cha 4: Baptist Mission Church – Magomeni

Kliniki zote hizi zitakuwa zinaanza saa nne asubuhi mpaka saa kumi jioni

Donnie Moen kuhudumu

No comments:

Post a Comment