Home

Wednesday, October 17, 2012

Joyous Celebration Kurekodi Joyous 17 tarehe 15/12/2012



Joyous Celebration on stage
Kundi maarufu la Joyous Celebration mnamo tarehe 15/12/2012 linatarajia kurekodi album yao mpya ijulikanayo kama Joyous 17.Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya kundi hilo Joyous watarekodi album hiyo pasipo kuwepo aliyekuwa Music Director wa kundi hilo Minister Nqubeko kitendo ambacho ni new experience kwao.Live recording hiyo inatarajiwa kufanyika katika ukumbi wa Rhema auditorium randburg na shughuli hiyo itaanza saa moja na nusu usiku na kiingilio ni randi 150 mpaka 300 ambazo ni sawa na 27,229.45/= mpaka 54458.90/= za Kitanzania

Pamoja na hatua hii ya MTN Joyous Celebration, lakini bado kuna mwangwi ndani ya mashabiki wa kundi hilo ambao wao wanaamini kitendo cha kutoa album mara kwa mara pasipo kujipanga kinapunguza ubora wa album zao.Pamoja na malalamiko hayo mmoja wa viongozi wa kundi hilo Lindelani Mkhize( mzee wa Kofia) amekuwa  akiwatoa hofu mashabiki kwa kusema wanajua wanachofanya.Wakati wa kurekodi Joyous 17 kundi hilo linatarajia kupanda jukwaani na member wake wote wapatao 45 wakiwamo waimbaji pamoja na bendi.Kwa experince ndogo utagundua kuwa tangu enzi za Joyous 5 iliyoitwa  mwaka 2001 mpaka leo 2012 Joyous wamekuwa wakirekodi LIVE DVD kila mwaka.

No comments:

Post a Comment