Home

Saturday, October 27, 2012

Night of Worship yawabariki wengi





John Lisu akihudumu katika ya Night of Worship

Usiku wa jana katika kanisa la Upanga City Christian Centre kulifanyika usiku wa kuabudu(Night of Worship) ambao ndani yake kuliwajumuisha wanamuziki na makundi mengi ya muziki wa injili toka ndani na nje ya nchi.Tukio zima lilianza kama kwenye saa tatu na nusu likiongozwa na Ma Mc wawili, Minister Samuel(Sam) wa CCC pamoja na Pastor Paul Safari.

Praise and worship team ya VCCT ni moja ya makundi yaliyopanda madhabahuni mapema,VCCT Praise Team ikiongozwa na Mpelo Kapama iliwaacha watu hoi kwa namna ilivyojipanga on stage.Kuna kwenda kuhudumu na kuna kujipanga kabla haujaenda kuihudumia mioyo ya watu, hawa watumishi kuanzia vocal, uchezaji on stage pamoja na uniformity katika uchezaji wao ni moja ya vitu vilivyowatofautisha wao na makundi mengine.Ni nadra sana kumuona Sam “Solo” Yona akilead jana aliimba nyimbo nzima tena sebene.


VCCT Praise team on stage
John Lisu pamoja na wanamuziki wake ni mmoja kati ya waimbaji ambao Mungu ametubariki nao nchini, naweza sema kwenye concert yoyote hapa nchini hususani Dar es Salaam ukiona viti havina watu pasi na shaka basi Lisu atakuwa akihudumu muda huo.Lisu aliimba YU HAI JEHOVA  kuufanya umati wote kuzama, huku Sam Yona, Masanja, Amani kapama,na wengine wakipiga ala za muziki.


Bupe on Stage

On the way from Kenya bro BUPE alipanda stejini na kuhudumu, Hosanna Inc imewahi kutana na wanamuziki wengi wanaofanya Gospel Hip Hop but Bupe he is blessed.Sifa moja ya Bupe ni kuwa huichukua Biblia na kui-turn through his art(Rap) na kuwa Mashairi.Bupe huku akifanyiwa back up na waimbaji zaidi ya MIA HAMSINI(makundi karibu tisa ya Praise and worship toka makanisa mbalimbali) aliuelezea ukuu wa Mungu kupitia Hip hop na kuwatoa tongotongo wengi kuwa Hip Hop madhabahuni nayo inakaa.
Glorious Celebration warekodi DVD LIVE

Kundi la Glorious Celebration(GC) linaloongozwa na Emmanuel Mabisa(Lindelani Mkhize), usiku wa jana kupitia Night of Worship(N.O.W) lilikuwa na kazi moja tu kurekodi LIVE DVD ya album yao mpya.Kazi ya kurekodi ilifanywa na Haak Neel production crew ambayo kwa sasa ndio bora kwa kurekodi LIVE chini, Haak Neel ndio waliorekodi DVD ya SIFA ZIVUME miaka kadhaa iliyopita pale Mlimani City.Ni wazi GC walikuwa wamejipanga vya kutosha licha ya kasoro ndogo ndogo,kwa yeyote alioona kazi ya GC madhabahuni atakiri kwamba kuna Mahari Mungu anaipeleka Tanzania kwa habari ya uimbaji.
Gc walikuwa na Round Mbili,walivyoanza round ya kwanza waliaza kwa kuimba tenzi kama mbili hivi kisha wakaanza kuimba nyimbo zao za kuabudu.

 Kaka Paul wa GC aliimba nyimbo iliyogusa mioyo ya wengii iitwayo UMENIFANYA IBADA na Mabisa pia aliimba tena NIGUSE,wakati wimbo wa Niguse ukiimbwa wengi walikuwa wakijiuliza ni mabiinti gani wa GC wata-cover nafasi ya Angel Benard na Jesca Honore ambao kwa sasa hawako na kundi hilo?, jibu la swali hilo lilipatikana na kuwaacha watu vinywa wazi.Kuna binti Hosanna Inc haikupata jina lake mara moja huyo mdada ali-cover  vilivyo sauti ya Angel huku Mercy Denis naye aliimba  kipande cha Jesca.
Glorious Celebration

Kashi Kashi zilianza pale kwenye round ya pili pindi GC waliposhift kutoka Kuabudu na kuanza Kusifu, Dany Kimambe aliiufanya umati mzima kusimama na kuimba naye wimbo wake wa JEHOVA, baada ya Dany akapanda mkaka wa kundi hilo aitwaye George,camoooon George aliimba SEBENE IPASAVYO.kwa kila mtu aliyewaona GC jana anayo habari ya ile STANDARD SEBENE kitendo ambacho kilichoniachia swali kuwa hawa ni Glorious Celebration au Glorious Sebene!!! (just a joke).


No comments:

Post a Comment