Home

Friday, October 12, 2012

Pamoja na kuvunjika kwa ndoa ya Sarah Jakes(Binti wa Td Jakes),wengi wampongeza binti huyo.


Td Jakes na bintiye
Sarah Dexter Jakes Binti wa Askofu mashuhuri Duniani Bishoip TD Jakes alikuwa mmoja wa watu waliowashangaza wanawake waliohudhuria kongamano la kihistoria liitwalo Woman Though art Loosed lililomalizika siku kadhaa zilizopita.Katika kongamano hilo ambalo kwa mwaka huu limefikisha miaka 20 limehudhuriwa na zaidi ya wanawake 25,000 kutoka sehemu mbalimbali duniani.

Katika Kongamano hilo Sara aliongea siku ya mwisho na moja kati ya mambo aloyoyasema ni pamoja na experience yake akiwa kama mwanamke, alikuwa muwazi kwa kuonyesha kuwa yeye sio perfect na alieleza ups and downs alizopitia na  akasema ametambua yeye ni nani.Kuyaweka bayana maisha yake kuliwafanya wengi kumpongeza kupitia facebook page na blogsite yake ikiwa ni ishara ya ukomavu.

Wakati akitangaza kuvunjika kwa ndoa miezi kadhaa iliyopita Sara Jakes alisema “kwa muda wa miaka minne niliyokuwa kwenye ndoa, nimejenga huduma yangu na nimekuwa mama na mke bora kadri nlivyoweza, kwa muda mrefu nimekuwa nikipitia katika mambo magumu na hii ni kwa kuwa nilitaka ndoa yangu idumu lakini imeshindikana”.Kwa sasa  Sarah ndiye kiongozi wa huduma ya wanawake katika kanisa la Potters House linaloongozwa na babaye Bishop TD Jakes

Sarah na mumwe siku ya Harusi yao
Sarah mwenye miaka 24 kwa sasa aliolewa na mchezaji wa zamani wa mchezo wa Ruggby aitwaye  Robert Henson ndoa iliyofungwa na Askofu maarufu duniani na swahiba wa Jakes  Bishop Noel Jones.Sarah na wamebahatika kupata mtoto mmoja wa kike

Wakati akitangaza ku-divorce Sara aliwahi sema  “After professional counselling, and prayerful consideration I have decided to end my four-year marriage. There are biblical grounds supporting this decision and I have attempted every other recourse but after multiple infractions over the course of the union, and for my personal safety and that of my children, I have come to this painful decision”

Kushoto ni Bishop Noel Jones,Td na Mkewe Sarita,Sarah na mumwe siku ya Harusi Sarah

No comments:

Post a Comment