Home

Wednesday, November 14, 2012

Mbowe Achangisha Milioni Kumi Kwa Ajili Ya Ujenzi Wa Mabweni Ya Shule Ya Kanisa


Awashukia Wanasiasa Wanaoendekeza Itikadi Zao Hadi Kwenye Makanisa Na Michango Yake


Mh Freeeman mbowe

MWEYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA) Freeeman mbowe amewataka wanasiasa kuachana na tabia ya kupeleka itikadi zao za kisiasa hadi ndani ya makanisa kwa kuwa itikadi hizo za kisiasa zinaonekana kushamiri hata kwenye baadhi ya makanisa na hivyo kunyima maendeleo ingawaje wanasiasa hao wana nafasi kubwa sana ya kuchangia

Mbowe aliyasema hayo wiki iliyopita katika harambee maalumu ya kuchangia mabweni ya shule ya Ufundi yaOlikii ambayo ipo chini ya kanisa la KKKT Dayosisi ya kaskazini kati ambapo pia katika harambee hiyo jumla ya Milioni 10 ziliweza kupatikana

Alisema kuwa inashangaza sana kuona kuwa baadhi ya wanasisasa wanashindwa kuchangia shuguli mbalimbali za maendeleo ya kanisa au kushiriki hata kwa pamoja katika kuchangia michango au kuendesha harambee kwa kuhofia kukutwa na Mwanasiasa mwingine jambo ambalo kama litaendelea hivyo basi litasababisha kabisa maendeleo ya kanisa kuwa hafifu sana


Aliongeza kuwa wanasisa wanapswa kujua na kutambua kuwa ni wajibu wao hata kuhakikisha kuwa wanakuwa sehemu ya kanisa  kwa kuweza kuendesha shuguli mbalimbali za maendeleo hasa katika ujenzi wa makanisa pamoja na mambo ya msingi ambayo yanafanywa na kanisa la leo ambapo kwa sasa bado hali ya kiitikadi inaendelea kushamiri ndani ya makanisa

Alifafanua kuwa hali hiyo pamoja na kuwa si njema sana kwa maendeleo ya kanisa kama itaendelea hivyo itasababisha kasi ya  kumjua Mungu hasa katika siasa hizo itapungua sana na badala yake kasi hiyo itaelekezwa zaidi katika mapabano ambayo hayana maana huku mapambano hayo huenda hata yakasabisha sana baadhi ya watu kukosa Amani dhidi ya wanasiasa hao

“inashangaza sana leo mimi kama Mbowe nikionekana mahala hapa ambapo ni patakatifu basi mtu wa CCM haji wala hashiriki kabisa sasa je tunajenga taifa la Kichadema au Ki CCM hapa na hali hii si hali ya kuendelea kuingalia kwa macho yetu bali hali hii inatakiwa kuangaliwa hata na viongozi wa dini wasimame vizuri na hata ikiwezekana waombe si jambo zuri  kwani kama ni Siasa basi zisiingizwe itikadi hadi ndani ya makanisa yetu kwani pia hali hiyo inasababisha tuyabomoe na wala sio kuyjenga;’aliongeza Mbowe

Katika hatua nyingine alisema kuwa nao wanasiasa ambao wanangangani itikadi za kivyama wanapaswa kujua na kutambua kuwa kamwe hawapaswi kufunga ndoa na vyama vya kisasa bali wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanakuwa wazalendo wa vyama vyao na kamwe itikadi kati ya CCM na Chadema isisababishe wakashindwa kutumikia Taifa hasa kwa Upande wa Makanisa yao.

Awali Meneja wa Shule hiyo ya Sekondari na Ufundi ya Olikii Mchungaji Izack Kisiri alisema kuwa lengo halisi la kufanya Harambee hiyo ambayo imefanikiwa kukusanya kiasi cha Zaidi ya Milioni 10 ni kuendeleza Mabweni kwa wanafunzi wa shule hiyo ili kuimarisha zaidi elimu

Mchungaji Kisiri alisema kuwa pamoja na kuwa wamefanikiwa kupata zaidi ya Milioni 10 lakini bado shule hiyo ina hiuitaji mkubwa sana wa mabweni kwani endapo kama kutakuwa na Mabweni ya kutosha  basi itaweza kuongeza sana hata kiwango cha elimu hasa katika eneo hilo la Olokii  ambalo bado lina uhitaji mkubwa sana .

‘tunafikiria kukusanya kiasi cha Shilingi Milioni 250 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni mawili lakini kwa awamu hii ya kwanza tunashukuru Mungu tumepata hii Milioni 10 lakini tunawatia Moyo wakristo na wadau wengine wa elimu kuhakikisha kuwa wanatuunga mkono na kuweza kuimarisha elimu  hasa kwa kuwa na mabweni  imara”aliongeza Mchungaji Kisiri.


Awali Askofu wa kanisa la kiinjili la kilutheri mkoani hapa( KKKT)dayosisi ya Kaskazini Kati Dkt Thomas Laizer alisema kuwa ni jambo la ajabu sana kwa wanasiasa kuchukiana ovyo kwa kuwa siasa inaenda kama mchezo wa mpira ambao kamwe hautabiriki na hivyo wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanajijengea tabia ya kupenda na kuthaminiana wao kwa wao hasa kwenye majukumu ya msingi ya Kimaendeleo.

Dkt Thomas alisema kuwa wapinzani kuwakataa watawala na watawala kuwakataa wapinzani si jambo jema na halitakiwi kuendelezwa kwa sasa kwani wote wanatakiwa kuhakikisha kuwa wanakuwa kitu kimoja na kutatua matatizo mbalimbali ambayo yanaikabili jamii kwa  sasa likiwemo suala zima la uvunjifu wa amani ndani ya Nchi.

Na Bety Alex, MERU

No comments:

Post a Comment