Home

Sunday, February 27, 2011

MAISHA NA HATIMA YA WANAFUNZI WA KRISTO MARA BAADA YA KRISTO KUONDOKA

Jiji la Jerusaleem ambapo Yakobo Mwana wa Zebedayo aliuwawa wakati akihubiri habari za Kristo
Leo katika Hosanna Inc tunapitia maisha ya wanafunzi wa kristo na wajibu waliopewa na kristo baada ya kristo kuondoka. Lengo hasa ni kutuwezesha kujua namna ambavyo waliotutangulia katika wokovu walivyokutana na changamoto ili na sisi tupige mbio zaidi katika kuutangaza ufalme wa Mungu. Hii ni kwa kua tumepokea hiki kijiti toka kwao hivyo na sisi tunayo safari yetu katika kristo YESU. Habari kuhusu Maisha ya Mitume hao na namna walivyosambaa duniani kote mpaka vifo vyao zinapatikana katika vitabu vilivyoandikwa katika kanisa la Kwanza. Schumacher ni Mwanahistoria wa kanisa aliyefanya utafiti kuhusu maisha ya mitume (wanafunzi wa kristo) na hivi ni namna ambavyo mitume hao walivyokuimbana na misukosuko katika kumtangaza Kristo Yesu.

MATHAYO
Mtumishi Mathayo yeye aliuwawa kwa upanga akiwa katika nchi ya Ethiopia

MARKO
Marko yeye alifia katika mji wa Alexandria nchini Misri mara baada ya kuburutwa na Farasi katika mitaa ya mji huo mpaka mauti ilipomfika.

LUKA
Yeye aliuwawa huko nchini ugiriki alipokua akitangaza habari za kristo

YOHANA
Yohana yeye aliwekwa katika kikaango/sinia kubwa lenye mafuta yaliyochemshwa na kwa Neema ya ajabu akafanikiwa kutoka katika mauti iliyokua ikimkabili.Baada ya kutoka katika kisiwa cha Patmo alipokua amefungwa na kufanikiwa kuandika kitabu chaUFUNUO akiwa kisiwani hapo, alikuja kua Askofu wa Edessa ambayo sasa inajulikana kama nchi ya Uturuki.Yohana alifariki nakiwa mzee sana na ni  mwanafunzi wa kristo pekee aliyekufa pasipo mateso.

PETRO
Yeye baada ya kukamatwa akieneza habari za Kristo, aliamriwa asulubiwe kichwa chini miguu juu kama Kristo Yesu, Lakini petro aliwaomba watu hao wamsimsulubishe kama namna ambavyo kristo alifanyiwa kwa kua Petro alisema yeye hana hadhi ya kusulubishwa kama Bwana wake. Ndipo walipoamua kumsulubisha kinyume na Kristo, hivyo Petro akasulubiwa kichwa chini miguu juu mpaka mauti ilipomfika.
Ramani ya jiji la Jerusalem
YAKOBO
Yeye alikua kiongozi wa kanisa la Yerusaremu, alitupwa katika bonde la mita mia moja pale alipokataa kuikana imani ya Kristo.Walipogundua kua hajafa adui zake waliamua kumpiga kwa rungu mpaka kufa. Bonde hilo ni lile ambalo Shetani alimuonyesha Yesu wakati akimjaribu kule nyikani.

YAKOBO MWANA WA ZEBEDAYO
Yeye alikua mvuvi kabla hajaitwa na kristo yeye iliuawa katka jiji la Jerusalem

BATHOLOMAYO
Alijulikana pia kwajina la Nathania ,alikua ni mmishionari katika bara la Asia, Alishuhudia habari za kristo katika nchi ya Uturuki.Aliuawa kwa kukaangwa.

ANDREA
Yeye  alitundikwa msalabani kwa mfumo wa X katika mji wa Patras nchini ugiriki baada ya kuteswa ipasavyo na askari wapatao saba,kasha wakamfunga msalabani with cords to plorong his agony.Wafuasi wake walisema  wakati wanampeleka msalabani,Andrea alisema “Nina uamuzi udumuo na niliutegemea muda huu wa furaha”. Aliendelea kuhubiri akiwa hapo msalabani kwa siku mbili mpaka pumzi yake ya mwisho ilipokoma

THOMASO
Yeye aliuawa kwa kuchomwa na mkuki huko India alipokua katika moja ya safari zake za kiumishieni kwa ajili ya kufungua kanisa.
Geti la kuingilia mji wa Damaskus huko Israel
                                                                                                                                                        

No comments:

Post a Comment