Home

Wednesday, March 23, 2011

HISTORIA YA MWANAMUZIKI WA INJILI EPHRAIM SEKELETI MUTALANGE


Ephraim Sekeleti
Ephraim Sekeleti Mutalange ni muimbaji maarufu wa nyimbo za Injili nchini Zambia, alizaliwa Mwaka 1983 katika mji wa Kalulushi nchini Zambia. Alimaliza elimu yake ya sekondari katika shule ya Kalulushi mwaka 2001.

Ephraim ni mtoto wa pili toka mwisho kati ya watoto sita, aliingia kwenye muziki wa injili tangu akiwa kinda huku alifundishwa kupiga kinanda na mmishonari alipokuwa bado mdogo. Mama yake anasema  “ Ephraim alikuwa ni mtoto aliyekuwa wa kelele nyingi”. Yeye pamoja na dada zake waliimba kanisani wakitumia kinanda na huko alipata uzoefu katika uimbaji na upigaji wa kinanda. Baadaye alijiendeleza katika uimbaji kwenye kikundi kilichojulikana kwa jina la  “Virtue for Christ” na aliimba katika kikundi hicho kwa muda wa miaka miwili.
Ephraim akiimba katika ibada ya kanisa la redeemed christian nchini Australia
 Mwaka 2002 akiwa na kiu ya kurekodi album yake, Aliamua kujitoa muhanga kwenda Afrika ya Kusini kwa kutumia kiasi kidogo tu cha pesa alichokuwa nacho, nia ilikua ni kurekodi album yake ya kwanza. Pamoja na jitihada hizo, baada ya kufika nchini Afrika ya Kusini alijikuta anaweza kurekodi nyimbo mbili tu kati ya album nzima. Hivyo akaamua kujiingiza katika Theater ya Pretoria na ndipo akapata fursa ya kuimba mbele ya Rais wa Afrika ya Kusini. Nafasi nyingi ziliendelea kujitokeza zilizomsababishia kutaka kuacha kuendelea na muziki wa injili ili aimbe miziki ya kidunia, lakini akawa muaminifu kuendelea na uimbaji wa injili. Mlango ulifunguka kumruhusu kurekodi album ya kwanza iitwayo Temba Baby“(Mtoto wa Miujiza)”.

Baada ya kurekodi, na kuuza nakala za kutosha za album hiyo ya Temba boy, kwa mafanikio ya hiyo kazi Ephraim aliamua kurudi nyumbani kuwekeza ile fedha. aliona awekeze zaidi kwenye ya album yake ya pili iliyopata mafanikio makubwa iliyoitwa Limo Ndanaka. Hi album imefanya vizuri kwenye chati mbalibali za muziki wa injili. Ephraim akiwa nje ya Zambia ameimba katika nchi mbali mbali zikiwemo Namibia, Afrika ya Kusini, Tanzania, Zimbawe na Australia.

Ephraim akiwa na mkewe Faith Mutalange
   
Alisema anafurahi akiona watu wasiokuwa na tumaina la Kristo wakianza kuwa na matumain, Licha ya kufanya muziki wake nchini Zambia amewahi kuja nchini Tanzania na kurekodi album yake nzima kwa Lugha ya Kiswahili. Moja kati ya Nyimbo zake zinazotamba hapa nchini ni pamoja na
Binti wa Ephraim

                                             1. Uniongoze                                 
                                             2. Baraka Zako
                                             3. Huu Mwaka 
 
 Ephraim hajui Kiswahili fasaha na nyimbo zake hizo alifundishwa kuziimba kwa lugha ya Kiswahili na Mchungaji ambaye pia ni muimbaji wa nyimbo za Injili kutoka Tanzania Ency Mwalukasa. Ephraim amesema ataendelea kuhubiri kwa njia ya uimbaji kwa sababu imempa changamoto zilizomuinua. Licha ya uimbaji Ephraim amefunga ndoa na Faith Chelishe na wamejaliwa kupata mtoto mmoja wa kike

                                                                                                                                                        


Ephraim na Faith
           
     ALBUM YAKE MPYA YA KISWAHILI IITWAYO VIGELEGELE

Wiki iliopita Hosanna Inc ilipata nafasi ya kuwasiliana na Ephraim Sekeleti akiwa Zambia, Alisema kwa sasa yuko katika hatua za Mwisho kukamilisha Album yake mpya itakayoitwa VIGELEGELE. Alisema anatarajia atakapokuja chini kwa ajili ya Tamasha la Pasaka atakuja nayo ikiwa imekamilika 

                               Moja kati ya kazi za Ephraim                                      

No comments:

Post a Comment