Home

Wednesday, March 23, 2011

KWA NINI MIKUTANO YA INJILI KWA SIKU HIZI HAINA HAMASA KAMA ZAMANI



Mwishoni mwa Miaka ya 1970 na Mwishoni mwa Miaka ya 1980 njia kuu iliyokuwa ikitumika kuwaleta watu kwa Yesu ilikuwa ni Mikutano Ya Injili ya hadhara ambapo watu wengi walimpokea Yesu kupitia mikutano hiyo. Wahubiri wa kizazi hicho, Mzee Emmanuel Lazaro, Mzee Moses Kulola, Mzee Kiwia, Mzee Kuselya a.k.a Toboa Tobo, Mzee Mpayo na Mzee Mwasumbi walikuwa na kazi kubwa ya kueneza neno la Mungu na asilimia kubwa ya watu waliookoka katika zama hizo waliokoka kwenye mikutano ya wahubiri hawa.


Bro Samuel Sasali
Miaka ya 80, ikaanzishwa huduma inaitwa “The Big November Crusades” chini ya Mzee Lutembeka na Mzee Kisondo. Mikutano hii ilikuwa na nguvu sana miaka hiyo. Nakumbuka yika katika maeneo ya Mnazi Mmoja na Jangwani kwa sisi wakazi wa Dar, Wagonjwa walikuwa wanaletwa kutoka Muhimbili na walikuwa wakirudi wamepona. 


Kwa mara ya Kwanza kwenye maisha yangu nakumbuka Mtu aliyekuwa kilema akiitwa Salvatory aliyeombewa na mchungaji George Gichana kutoka Kenya ali maarufu “GG” na kutembea kabisaa, nakumbuka enzi hizo pamoja na Mzee Roy Dama walikuwa wakija Dar-es-Salaam, kila shughuli ilikuwa inasimama na kila mtu akisubiria “The Big November” ili kuona miujiza lakini pia kuona kwaya kuu zilizokuwa zikitamba enzi hizo, Mtoni Lutheran, na wimbo wao wa Lulu, Chini ya Mwl. George Victory Singers na Wimbo wao wa Mchakamchaka, Chini ya Mwalimu Mwalubalile na Revival Singers na wimbo wao uko wapi, chini ya Mwalimu Mackenzie






Miaka ya 90 na Mpaka sasa nimeona kama hii mikutano ya injili ya hadhara imekuwa kama haina matokeo mazuri ama makubwa kuliko katika kizazi kile cha Mwishoni    mwa , 2010 niliamua kutembelea katika baadhi ya mikutano ya injili iliyokuwa inafanyika Dar, nilitembelea pale kabisa la Kibaptisti pale Kinondoni, Kisha nikahudhuria mkutano wa injili pale Biafra,nikahudhuria mkutano wa injili kule maeneo ya Boko Basihaya na mkutano mwingine maeneo ya Sinza na pia KKKT kule Wazo hili Kilichokuwa kinanisukuma kutazama mikutano hii ni kutaka pia kuona mikutano hii inavyoendeshwa, mwitikio wa waumini wenyewe kwenye mikutano hii, na pia mpango mkakati wa kuwatunza hawa wanaoamua kumpa Yesu Maisha yao.
                           
Askofu Moses Kulola moja kati ya wahubiri maarufu waliookoa na kuponya nafsi za wengi kupitia mikutano ya Injili
Mbali na mikutano ya injili, pia nimekuwa nikiwasikiliza watumishi wa Mungu wale wanaohubiri kwenye vituo vya mabasi, pale Posta kuna rafiki yangu huwa anahubiri, mwenge kituoni kuna mpendwa huwa anahubiri, stendi ya mkoa kuwa wanaohubiri na kuna wengine wanakusanya sadaka kabisaaaa kwa ajili ya kupata maomb meona kwenye kuangalia kwangu ni kama ifuatavyo   




Mbali na mikutano ya injili, pia nimekuwa nikiwasikiliza watumishi wa Mungu wale wanaohubiri kwenye vituo vya mabasi, pale Posta kuna rafiki yangu huwa anahubiri, mwenge kituoni kuna mpendwa huwa anahubiri, stendi ya mkoa kuwa wanaohubiri na kuna wengine wanakusanya sadaka kabisaaaa kwa ajili ya kupata maomb meona kwenye kuangalia kwangu ni kama ifuatavyo.

Mamia ya watu wakiwa katika Mkutano wa nje wa Injili
                                                                       
 Mikutano Ya Injili.

1. Waumini wengi (wenyeji) wa mikutano wanapatika siku za Jumamosi na Jumapili, siku za kawaida mikutano huwa na watu wachache na kukosa hamasa ya watu.

2. Mkutano Mingi inayowekwa kwenye viwanja vya makanisa huwa na washirika zaidi kuliko wenye dhambi katika kuhudhuria. Ikifika saa ya kukata shauri muhubiri hutumia muda mrefu wa kuamua kuimba pambiodent:-

3. Wahudumu wengi wa Mikutano wanakuwa hawako well trained kwa ajili ya hiyo kazi, Mfn. Namna ya kukaribisha watu, namna ya kubeba wagonjwa, namna ya kukemea mapepo na pia namna ya kusimama katika kuombea watu, kila Muhubiri ana style yake ya wahudumu kusimama.

4. Mikutano inayofanyikia kama Jangwani, Biafra, Kawe au katika viwanja vya wazi ni ngumu kuwapata wale kondoo wapya kutokana na umbali wa viwanja na makazi ya watu pia.

Wengi wanaohudhuria mikutano hii ni watu wa hali ya chini, wale wasiokuwa na kazi, wafanyakazi wa ndani na wanafunzi. Watu ambao ni wafanyakazi wengi wanatingwa na miundo mbinu ya barabara inapelekea wao kuchelewa kuwasili maeneo ya mikutano

6. Waongofu wapya wengi huwa hawadumu, unaweza kuta waliookoka jumla ni 100, wanaoendelea mpaka sasa ni wawili.

7. Wahubiri wengi wanje wanaongea vizu a lakini ile nguvu ya udhihirisho ni ndogo sana, yaani wagonjwa kupona wengi ni wale wa tumbo, kichwa na maumivu tu. Ila vipofu, vilema na viziwi bado imekuwa utata kuwapata waliofunguka

8. Ile tabia ya watu kukata shauri na kuhamia kwenye “dhehebu” wenye kuhost mkutano imepitwa na wakati. Wengi wanaokoka na kubaki huko huko waliko ambapo imepelekea kupunguza morale ya “kuwavunia” wengine na makanisa kuamua ku-opt “Semina Za Ndani”.

9. Waumini wengi si wepesi wa wenda nao zaidi ya wenyeweji kujazana wenyewe uwanjani


Muinjilisti Reinhard Bonke ni moja kati ya wamishionari walioleta maelfu ya watu kwa kristo kupitia Mikutano ya nje ya Injili


Wahubiri wa Kwenye Vituo Vya Mabasi
  


1. Wengi wa wahubiri hawa hawajaribu kuonesha upendo wa Mungu, ila kuwatuhumu abiria na kuwaogopesha na siku ya mwisho. Nimewahi kumsikia Muhubiri pale Posta akiongelea mavazi na wakati mwingine hata Dowans katikati ya Mahubiri.

2. Muhubiri anapokanza kuhubiri wanaomsikia ni wengine, mpaka ikifik kata shauri ni mara chache mtu akakaa kituo cha basi zaidi ya nusu saa kusikiliza mahubiri kuliko mtu kusikiliza sauti ya konda anapoita abiria

3. Mpango Mzima wa sadaka sijajua kama wale watumishi wanakumbuka kutoa kikumi, maana akichukua kila basi per day ana make inaweza kumfanya akaona ile ndo ajira yake ya kila siku, kuhubiri na kukusanya sadaka

Lazima nikiri kuwa kuhubiri katika hadhara pia ina faida sana kwenye maisha ya waamini, inakujenga na kukupa ujasiri. Kwa sisi ambao tumekuwa bega kwa bega na wazee wetu kwenye mikutano ya injili, lazima tukiri mikutano ya injili ya nje inakujenga kimwili na kiroho na kisaikolojia pia.

Kwa changamoto nilizozitaja kwangu naona mikutano ya injili inahitaji kutazamwa upya kwa maana ya namna tunavyotumia rasilimali tulizonazo, muda, fedha, watu na kila kilichopo. Semina za Kiroho ambazo zimekuwa zikijenga hata wapendwa nimebaini zimekuwa natokeo makubwa kuliko mikutano ambayo Kanisa linatumia gharama kubwa kuliko matunda ya mikutano hii. Nadhani ipo haja ya sisi wadau kusaidia kuliona hili na pia kushauri pale tunapopaswa kushauri                                                                                                                     
Wasalaam,
Samuel Sasali Papaa

 Coments za Watumishi wengine Kuhusu mikutano ya nje ya Injili 

Bro Edmund Mugasha
Kweli mikutano ya nje imepungua na hii mi naona ni kusababishwa na mazingira nikimaanisha mikutano mingi ya zamani ilibase kwenye injili haswa na watu kuokoa, kwasasa mingiimeamiakwenye semina na semina nyingi kufanya na wenyehudumaya kialimu na mitume,pia naona imeamia kwenye majengo ya ndani nikimaanisha makanisa na mahema. 

Kingine naona ni wale wainjilisti wa zamani waliokuwakwenye majukwaa na viwanjani hawakuandaa watu kipindi walichokuwepo ili ikitokea hawapo au kipindi chao cha kazi kumalizika basi gurudumu litabebwa na hao walioachiwa. 

Finally kwangumimi naona ni swala la season kwa sasa Mungu anatumia huduma ya kialimu sana kuwafundisha watu neno badala ya forces za wainjilisti. 

Lakiniinabidi kukutana na wainjilisti hawa wa zamani ni rahisikupata views zao katikahili na pia tazama vijana wa sasa nguvu na upako wakiinjilisti umepoa sana kwao wote wanabase kwenye miracles,unabii na n.k


Annonimus

Kwa mimi nahisî msukumo wa kuendelea na mikutano pia umepungua.
yawezekana ni :
1. kuongezeka waumini makanisa ya wale waliokuwa wanafanya mikutano hii ya injili ya nje.

2. mafundisho ya kiinjilisti yamepungua na hivyo kukosekana kwa wainjilisti wapya kuendeleza kazi.

3. Maendeleo ya kiteknolojia yanayofanya matumizi ya redio na tv kuwa makubwa na hivyo kuwafikia watu wengi zaidi kama vile afanyavyo mzee wa upako, mama lwakatare na kakobe. Hata miziki ya injili inavyozidi kuimarika na kuwafikia watu wengi kubadilisha maisha yao.



                 

2 comments:

  1. Kanisa lazima likubali kwenda na mabadiliko kwa sasa maana ulimwengu unabadailika, a church should think on how to use the advanced technology. Swali linanijia Kanisa ni nani??kama mimi na wewe basi hapa tulipo tunahubiri.

    Changamoto kubwa sana Kanisa linaona kama mambo haya ni ya dunia zaidi kuliko "kuhubiri" bara barani.

    ReplyDelete
  2. I sense selfishness and loss of direction. I should ask, wahubiri wa leo wajiulize yafuatayo:
    1. Nia ya mikutano ya nje leo na wakati ule. Kuna utofauti?Kwanini watu hufanya mikutano ya nje?
    2. Wahubiri wengi wameamua kuwa na makanisa yao, sasa anachokifanya kwenye mkutano wa nje hakitofautiani na anachokifanya kanisani. Suala linalokuja ni kwamba, wakristo wanaona kama kinachohubiriwa na namna kinavyohubiriwa ndani ni sawa na nje, kwanini kuvunja ratiba nyingine ilhali akija jumapili atakikuta? Kwa sababu ukweli ni huu: If kinachofanyika katika mikutano ya nje kina tija na kina utofauti (it is different, interesting and effective) watu wapo tayari kuvunja shughuli zao na kwenda. Mfano ni Tiba ya babu Loliondo ( simaanishi naunga mkono ama la, ila nasema tu) wangapi waliacha shughuli zao wakaenda loliondo tena kwa gharama kubwa na kwa safari ya siku kadhaa? Je, kipindi hicho cha nyuma mikutano ilipokuwa hot, wangapi waliacha shughuli zao na kuja kwenye mikutano?
    3. We need to learn 'Condor'. Wengi wetu hatujifunzi kuwa wawazi hata kama uwazi huu na ukweli haupendezi. Mimi ninaloliona siku hizi 'uvuvio or Holy Spirit presence imepungua katika mikutano mingi. Content ya mahubiri na namna yanavyohubiriwa leaves alot of questions. I have heard alot of blasphemy, kujisahau na kujikuta mhubiri anajitukuza yeye badala ya kutumkuza Mungu matokeo yake utukufu wa Mungu haushuki
    4. Nafasi ya kusifu na kuabudu na maandalizi kwa ujumla. Wakati huo, wahubiri walikuwa na nafasi nzuri ya kujiandaa na kufunga na kuomba kwa ajili ya mikutano husika. Siku hizi mambo mengi, muhubiri yeye mwenyewe ana kanisa lake, kuna mambo kibao anatakiwa kuyashughulikia halafu kuna mkutano. Muda wa kukuaa katika uwepo wa Mungu kwa ajili ya mkutano ni finyu sana. Pia, maandalizi ya mkutano, kwa kuimba na kuabudu ni finyu, ni huduma ambayo inakwenda chini sana - nikimaanisha waimbaji badala ya kuwa focused siku hizi kwenye kuugusa moyo wa Mungu kwa sifa wana-focus kwenye kujulikana na kujipatia sifa (unyenyekevu umepungua). Pia, wengi hawana habari kuwa kuimba nayo inahitaji maandalizi na kujiweka uweponimwa Mungu kwa muda mrefu. Matokeo yake, mwimbaji yupo madhabahuni lakini muda mfupi ametoka kuzini, kutamani, kulewa, kusengenya etc na hajafanya maandalizi ya moyo wake kwa mfano kutubu na kujitakasa kabla ya kupanda jukwaani. Matokeo yake watu wanasifu kwa mazoea. Uwepo wa Mungu unapungua. Pia, kutokana na mambo mengi katika ratiba, kusifu na kuabudu hakupewi muda wa kutosha, nyimbo mbili mbili tu eti kwisha! Jamani, watu wameshaau kusifu na kuabudu hadi mtu unasahau mambo ya kidunia inayokuzunguka. Siku hizi mtu anasifu na kuabudu huku anatuma msg kwenye simu ya mkononi, wapi na wapi?

    Mtizamo wangu ni kuwa sote - Wahubiri na wahubiriwa tumechangia kwa hili, sote tujipange upya kama tunahitaji kumrudisha Roo mtakatifu katika mikutano yetu.
    Ni hayo tu kwa leo
    (Jackson Luka Nkya - 0755 803 941)

    ReplyDelete