Home

Saturday, April 30, 2011

Matokeo ya Swali la mwezi wa April

Hapa katika Hosanna Inc kwa mwezi wa nne wote tumekuwa na swali tukitaka kujua  “Endapo nchi itakuwa na wabunge wengi waliookoka,  Je !!! hatua hiyo inasaidia nchi kuongozwa na Mungu ?"

Matokeo ya swali hilo yanaonyesha
5%  Walisema SIO KWELI
53% Walisema NI KWELI
31% Walisema SIO LAZIMA

Kila aliyepiga kura anazo sababu zake japokuwa wapo aliodai uwepo wa namba kubwa ya wabunge waliookoka is not a guarantee kwa nchi kuongozwa na Mungu.
Matokeo hayo yanadhihirisha kuwa wakristo wengi wanaimani ili nchi iongozwe na Mungu, inahitaji  idadi ya wabunge waliookoka iongezeke ili waweze kufanya maamuzi kirahisi yenye lengo la kuujenga mwili wa kristo.

Tunatoa shukrani za dhati kwa wasomaji wote wa Blog hii kwa kupiga kura katika swali hilo.Tunatarajia kuwa na swali lingine kuanzia jumatatu.

No comments:

Post a Comment