Home

Saturday, April 30, 2011

Ziara ya Mchungaji Daniel Kulola nchini Uingereza yazidi kufanikiwa

Mch Daniel Kulola akihudumu katika jiji la Manchester
Mnamo Tarehe 20/06/2011 Mch Daniel Kulola na Mkewe waliondoka nchini kuelekea nchini uingereza kwa ajili ya kupeleka Neno la Mungu. Tarehe 22-24 walianza kuhudumu Neno la Mungu katika jiji la Manchester ila kwa sasa wapo katika Mji wa Lancaster ampapo wanatarajia kumaliza semina ijumaa ijayo.

Mrs Daniel Kulola
Mchungaji Kulola ameiambia Hosanna Inc kuwa baada ya kutoka Lancaster anatarajia  kuendelea na huduma kwenye mji wa Milton Keynes Tarehe 6-8/05/2011
na Tarehe 8 hiyo hiyo watakuwa na Huduma katika jiji la Coventry.Kuanzia Tarehe 10-16/05/2011 watakuwa na huduma katika jiji la Birnmingharm pamoja na London, kisha Tarehe 20-23/05/2011 watakuwa wakifanya Huduma katika mji wa Reading.

Wakristo wakimsikiliza Mch Kulola, wa kwanza kulia ni Mrs Daniel Kulola
Mchungaji kulola amezidi kuiambia Hosanna Inc kuwa kwa sasa Waingereza wamekosa uamsho wa Injili ya Kweli, kitu ambacho kinawasumbua katika mwenendo wao wa Maisha ya  Kiroho. Mungu awabariki Mr. and Mrs. Daniel Kulola kwa kazi mnayoifanya

Mch Kulola akiwa na baadhi ya wakristo waliohudhuria semina, wa kwanza kulia waliosimama ni Sister Diana Madida Kihaile

No comments:

Post a Comment