Home

Saturday, April 30, 2011

Tunaishi ili kutimiza lengo la Mungu

Message from Altar

Isaya 43:1
"Lakini sasa, Bwana aliyekuhukumu, Eee Yakobo, yeye aliyekuumba, Ee Israel, asema hivi, Usiogope, maana nimekukomboa, nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu."

Maadamu Mungu amekupa Neema ya kuishi chini ya jua ina maana amekuona unafaa, na hakuna mbadala wako ndo mana akasema katika Isaya 43:1(i) anasema NIMEKUITA KWA JINA LAKO, anamaanisha  Kile ambacho Mungu amekiweka ndani yako kwa ajili ya utukufu wake, ni cha kipekee na hakuna mwanadamu mwingine chini ya jua mwenye uwezo wa kukitekeleza kama ambavyo wewe uwezavyo kukitekeleza.

Ukishalijua hilo kiasi cha kwamba akili, nyama,damu,moyo mpaka pumzi vikameza hilo kusudi la Mungu ndani yako, viwango vya utekelezaji wa kusudi hilo huwa vya hali ya juu. Ukifanikiwa kufika katika hatua hiyo kiufahamu hupelekea kila dakika moyo, nafsi, na mwili hujipima ufanisi wa utendaji wao katika kufanikisha hilo kusudi la Mungu. Ndio hatua ipelekeayo kuamini tunakula ili tuishi na sio tunaishi ili tule. Mali, mavazi Chakula na vyote ulivyonavyo vinakua kama sehemu ya kukusapot ili kufikia lengo la Mungu ndani yako.

Tunapofikia katika viwango hivyo kiutendaji ndipo altitudes zetu katika Mungu hubadilika na kumlingana yeye, hivyo hatutoweza kujivuna kwa ajili ya Mali tulizonazo kwa kuwa sio kusudi la kwanza la Mungu ndani yetu, hatutoweza kujivunia elimu tulizonayo kwa kuwa sio kusudi la msingi kwa sisi kuwa chini ya jua, bali haya mazidisho yote ni kwa ajili ya kutuwezesha kukamilisha kwa usahihi lile kusudi la msingi ambalo Mungu ameliweka kwa kila amwitaye Baba.

V.Mboya

No comments:

Post a Comment