Home

Wednesday, April 13, 2011

Mtume Ndegi alalamikia Injili kugeuzwa biashara

Mtume Onesmo Ndegi na Mkewe toka Living water kawe makuti
Mtume Onesmo Ndegi wa huduma ya Living water kawe  ya jijini Dar es salaam akiwa katika semina jijini arusha amesema, kwa sasa injili imevamiwa na  walanguzi kama wale kristo aliowatimua walipogeuza hekalu la Mungu kuwa pango la biashara.alikemea vikali tabia ya watumishi wa Mungu kujipatia kipato kwa njia ya kuwatabiria waumini. Mtumishi Ndegi aliwataka watumishi waache kukusanya mamilioni ya pesa kwa njia hiyo na badala yake wafanye kazi ya kuwafikisha watu mbinguni na si kujinufaisha wao. 

Alisema endapo Mchungaji anapotoa utabiri kisha akadai fedha ya kukombolewa anafanya vibaya, kwa kua Kristo alipotuweka huru hakudai chochote na leo inapotokea hivyo ni kuchanganya biashara na Biblia. Mtume Ndegi aliwataka wakristo kuwa makini na kuacha tabia ya kupenda kutabiriwa pamoja na unabii kwa kua kama wakikaa vizuri na Mungu Roho atawaongoza katika mema yote.

1 comment:

  1. Naomba salamu zangu zimfikie "My Dad". Shule yake huwa naikubali mbaya

    ReplyDelete