Home

Saturday, April 16, 2011

TAMASHA LA AFLEWO LATIKISA JIJI LA DAR-ES-SALAAM

Tamasha kubwa lililokuwa likisubiliwa kwa hamu na wakazi wa jiji la Dar-es-salaam liitwalo AFLEWO, jana katika ukumbi wa Diamond Jubelee lilifanyika kwa mafanikio makubwa. Aflewo yenye asili yake katika vyuo vikuu vya Kenya ikiwa na maana ya Africa Lets Worship lina lengo kubwa katika  kuwakutanisha waafrika toka nchi mbalimbali na kumwabudu Mungu pamoja. 

Katika  usiku wa jana watu wengi walijitokeza kumsifu na kumwabudu Mungu huku wachungaji waliohudhuria ukumbini hapo  akiwepo Dr Huruma Nkone, Mtume Onesmo Ndegi na Mlezi wa Aflewo Tanzania Mch Abel Orgnes  waliendesha maombi kwa watu wenye shida mbalimbali.

Kikosi kazi kilichoandaa Tukio zima la Aflewo Tanzania
Praise team ya Aflewo toka Kenya ikiwa Jukwaani  


Dr Huruma Nkone akifungua rasmi usiku wa Aflewo Tanzania,nyuma yake ni Praise Team ya Aflewo toka Tanzania  


Pastor Safari na John Kagaruki

John Lisu akiongoza Praise and worship team ya Aflewo Tanzania

Roho Mtakatifu akiwahudumia watuGlory be to GOD

Mtume Onesmo Ndegi na wachungaji wengine wakihudumia watu wenye mahitaji mbalimbali

Source: Samwel Papaa

No comments:

Post a Comment