Home

Monday, April 18, 2011

Discussion Board



Topic: Nini kinachosababisha makanisa mengi ya kipentekoste kuondokana na mfumo wa kuwa na kwaya na badala yake kuwa na Praise and Worship Team?
  
Kwa siku za usoni tumeshuhudia makanisa mengi hususani yakipentekoste yakiondokana na mfumo wa kuwa na kwaya nyingi kanisani na badala yake yameunda vikundi maalumu vya kusifu na kuabudu. Mabadilko haya yamekuwa yakishika kasi kila uchao hapa nchini Tanzania. Ni makanisa machache yakipentekoste ukiachilia mbali yakiprotestant   ambayo mpaka kesho bado yaendeleza taratibu za kuwa na kwaya.

Hosanna Inc chini ya kipengele cha Discussion Board inaanza kukusanya maoni ili kujua nini kinachopelekea hii hali kushamiri. Baada ya kukusanya maoni tutayaweka bayana hapahapa katika blog yako na mwisho wa kukusanya maoni ni ijumaa ijayo tar 22/04/2011. Unaweza changia maoni yako kupitia njia zifuatazo.

Email Address: victormboya@gmail.com

Phone No +255-754388

Message kupitia Facebook: Hosanna Inc - Tanzania

No comments:

Post a Comment