Home

Monday, April 18, 2011

Mchungaji Daniel Kulola kuondoka jumatano ijayo kuelekea nchini Uingereza

Mch Daniel Kulola
Muinjilisti na Mchungaji maarufu nchini Tanzania Mch Daniel Kulola pamoja na mkewe, jumatano ijayo tarehe 20/04/2011 anatarajia kuondoka nchini Tanzania na kwenda Uingereza katika jiji la Manchester kwa ajili ya kuhubiri Neno la Mungu. Muinjilisti  Daniel Kulola ambaye kwa sasa ni Mchungaji wa kanisa la EAGT Lumala katika jiji la mwanza, ameiambia Hosanna Inc kuwa jumapili ya jana tar 17/04/2011 alikua akiondoka jijini mwanza kuelekea Dar-es-salaam kwa ajili ya maandalizi ya safari hiyo.

Mtumish Daniel Kulola akihubiri katika moja ya mikutano ya Injili
                                                    
Akiwa nchini uingereza atahubiri katika semina iliyoandaliwa na Christians Tanzanians in Europe(ctie) Kuanzia tarehe 22april mpaka 24April 2011. Mchungaji Kulola amekuwa akipata mialiko mara kwa mara ya kuhubiri ndani na nje ya Tanzania. Yule Mungu aliyeianzisha kazi yake ndani ya Mchungaji Daniel kulola, ataifanikisha  kwa ukamilifu wake.

No comments:

Post a Comment