Home

Monday, April 18, 2011

Uche Chukwu Agu mwibaji wa nyimbo maarufu barani afrika iitwayo My GOD is good (Double Double)

Live Performance ya My GOD is Good kati ya Uche Agu na Kundi la Joyous Celebration
Uche Agu ni Mwanamuziki wa nyimbo za injili na raia wa Nigeria anyeishi nchini Afrika ya kusini, moja kati ya mafanikio yake ni kunyakua tuzo ya mwanamuziki bora wa nyimbo za injili barani afrika. Hivi sasa nyimbo yake ya My GOD is good oohh ambayo wengine huiita Double Double aliyoifanya na kundi maarufu la injili nchini afrika ya kusini liitwwalo JOYOUS CELEBRATION imesambaa Afrika nzima na imekuwa gumzo hali iliyomfanya kuwa maarufu kwa muda mfupi.

Uche anastashahada ya Theologia kutoka World Harvest Theological College na huongoza sifa na kuabudu katika huduma iitwayo Halleluya Ministry International yenye makazi yake nchini Afrika ya kusini katika jiji la Johanesbag. Tarehe 7 mwezi wa tatu mwaka huu alialikwa nchini Ghana katika tamasha kubwa la kipekee lililoiywa Independence Praize 2011

Vocalist Uchechwuku Agu

Uche akiwa ameshika tuzo mbili alizopewa na Africa Gospel Music Awards, moja kati ya tuzo hizo ni ile ya Mwanamuziki Bora wa muziki wa injili barani Afrika
 
Mwenyewe anaamini kuwa nyimbo zake zinaleta uhamsho na nguvu mpya kwa vijana na hivyo  kutengeneza kizazi kipya chenye hofu ya kumwabudu Mungu. Mwaka huu Katika tuzo za Muziki za nchini afrika ya kusini zijulikanazo kama  South Afrika Music Awards (sama), Uche amechaguliwa kugombea kategori ya Best African Contemporary Gospel Album. Tuzo hizo zinatarajiwa kufanyika nchini humo kati ya tarehe 20 au 21 mwezi ujao, miongoni mwa wanamuziki wa Injili wanaowania tuzo katika kategiri hiyo ni

Best African Contemporary Gospel Album                      
Benjamin Dube – Worship In His Presence
Group – Spirit Of Praise Vol 3
Mthunzi Namba – Mercy Live In Durban
Uche – Live At Lyric Theatre
Worship House – Worship House Project 7 - It Is Well With My Soul

Moja kati ya matangazo ya Matamasha ya Uche



Ifuatayo ni kazi nyingine ya Uche iitwayo Solid Rock





Everything is Double Double by Atta Boafo

Atta Boafo ni kijana wa kighana kutoka katika jimbo la Kumasi ambaye amekuja na nyimbo hiyo ya Double Double toka kwa Uche ila kwa staili yake mwenyewe. Kitanzania Tanzania tunaweza iita Remix, Boafo amesomea muziki kwa kipindi kirefu na nyimbo yake hiyo imesambaa sehemu nyingi pia barani afrika. Unaweza kuiona  Everything is Double Double by Atta Boafo kwa kuclick hii video hapo chini

No comments:

Post a Comment