Home

Tuesday, May 17, 2011

Benny Hinny and Paula White wazungumzia juu ya shutuma dhidi ya Mahusianoa yao


Watumishi wa Mungu maarufu Duniani Pastor Benny Hinny na Muinjilist mwanamama Paula White kila mmoja kupitia tovuti yake wameweka bayana juu ya mahusiano yao. Pastor Benny Hinny na Paula walipata shutuma nyingi toka kwa watu mbalimbali kuwa wako katika mahusiano ya kimapenzi. Hali hii ilitokana na jarida la National Enquirer tarehe 23 july mwaka jana kushapisha picha iliyowaonyesha Benn na Paula wakitoka katika Hoteli huku wakiwa mameshikana mikono.

Benny Hinny mwenye miaka 57 na Paula 44 wote kwa pamoja wameweka wazi kuwa wamekuwa marafiki kwa takribami miongo miwili, na mahusiano hayo yamekuwa ni kwa ajili ya kazi ya Mungu pekee na sio kinyume na hapo kama wengi wanavyo tafsiri. Kupitia tovuti zao kwa nyakati tofauti kila mmoja alinukuliwa akiacha ujumbe ufuatao.

Pastor Benny Hinny: Hakuna chochote ambacho kiko kinyume na mapenzi ya Mungu juu ya mahusiano kati yangu na Mtumishi Paula white
Ev Paula White: Tumekuwa marafiki kwa karibu sana kwa kuwa kila mmoja amepitia  katika maumvu ya kuvunjika kwa ndoa huku jamii nzima ikishuhudia. Ila pamoja na yote hayo uhusiano wangu na Benny Hinny kimwili na kiroho hauna doa mbele za Mungu


Source: Gospelnewswire

No comments:

Post a Comment