Home

Tuesday, May 17, 2011

Njia Rahisi ya Kuleta Upya katika Maisha yako


Inawezekana unaona maisha yako hayana msisimko na yamekuwa kama ‘routine’ fulani. Hakuna kitu kinachokufurahisha tena wala kukufanya uamke asubuhi kwa uchangamfu na kutazamia siku kwa furaha.

i) Tafuta kitu unachokipenda na ujifunze kwa wakati wa ziada, inaweza kuwa ni kupika keki, kufuma kitambaa, uchoraji wa picha, huduma ya kwanza, upambaji wa uso n.k chochote ambacho unaona kutakuchangamsha na kukupa ujuzi fulani.

ii) Endeleza vitu vinavyokupa furaha na kukufanya ujisikie kutiwa moyo na kufarijika. Kuwa na mahusiano mazuri na ndugu na marafiki, hudhuria semina za kukuinua na soma vitabu vya kukuimarisha.

iii) Ijali familia yako, uwe pamoja nayo katika furaha na huzuni zao, kuwa mwepesi kusamehe na kuachilia, uwe mkarimu na tayari kutoa msaada pale inapohitajika kwa upendo na furaha.

iv) Weka nyumba yako katika hali ya kuvutia. Chumba cha kulala kiwe kimepangiliwa vizuri, jiko liwe safi, sebule na mazingira yote ya nyumba yawe yanayokufanya ujisikie vizuri.

v) Jitolee kumfundisha mtu au watu kitu ambacho unajua kitawasaidia, mfano sunday school ya watoto, mapishi fulani ambayo wewe unayajua zaidi, kufundisha kwaya n.k. Unapomsaidia mtu kuelewa kitu kipya utaona maisha yako yakipata maana zaidi.

vi) Onyesha wema kwa watu zaidi ya ndugu na marafiki. Toa msaada kwa wenye mahitaji, angalia wajane na yatima hata kwa ushauri tu, mpishe mzee au mgonjwa siti kwenye daladala, mpe nafasi mjamzito awe mbele yako kwenye foleni benki au kwenye ATM.
Ubarikiwe!


Source: Women of Christ

No comments:

Post a Comment