Home

Sunday, May 1, 2011

Groove Awards Tour to Mombasa, Machakos and Nakuru

Grove awards ni tuzo maarufu zinazowahusisha wanamuziki wa muziki wa Injili nchini Kenya na Afrika mashariki kwa ujumla. Kabla ya kufanyika tuzo hizo mwaka mwaka baadhi ya wanamuziki waliochaguliwa katika kategori mbalimbali walipata fursa ya kufanya Tour (Ziara)  katika vituo mbalimbali vya watu wenye uhitaji na kuimba pamoja nao pia kufanya maombi pamoja nao. Ziara hiyo ilifanyika katika Miji ya Machakos,Mombasa na Nakuru. Rose Muhando na Christina Shusho waliiwakilisha Tanzania katika ziara hiyo.

Tuzo za muziki wa injili Tanzania zina mengi ya kujifunza kwa hawa jamaa

Katika mji wa Machakos Wanamuziki walipata nafasi ya kushiriki michezo na watoto wenye mahitaji mbalimbali

Walipata nafasi ya kuomba pamoja nao

Christina Shusho on STAGE katika ziara hiyo, 

Rose Mhando on Stage

Marion Shanko akiimba katika ziara hiyo

Pastor Peter Odanga akifundisha Neno la Mungu na kufanya Maombezi wakati wa ziara hiyo
 

No comments:

Post a Comment