Home

Saturday, May 7, 2011

Tusiwamiliki waumini wala Makanisa kama mali zetu binafsi


Mahali pa Ibada

Nashukuru kwa kunipa nafasi niweze toa maoni yangu. Paulo alisema naliuweka msingi wa mafundisho sahihi , na mwingine anajenga juu yake. Lakini kila mtu na aangalie anavyojenga juu yake .Maana msingi mwingine hakuna mtu awezaye kuuweka, isipokuwa ni ile iliyokwisha kuwwekwa yaani Yesu Kristo, 1Wakorintho 3:10-11.

Mungu hakukusudia mtu mmoja katika kanisa la mahali (local church) awe kila kitu. Mtume Paulo alisema “Lakini kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadri ya kipimo cha kipawa chake... Kristo alipopaa juu aliteka mateka, akawapa wanadamu vipawa wemgine kuwa Mitume, manabii, wainjilisti, wachungaji na waalimu. Kusudi kubwa la hayo yote ni kuwakamilisha  watakatifu ili kazi ya Mungu itendeke kwa ufasaha, hata mwili wa kristo ujengwe tikiwa na msimamo, Efeso 4:7-12 “ ili tusiwe tena watoto wachanga tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa Elimu…,

Katika kanisa la leo kuna mgongano wa kimaslahi kati ya Mungu na Viongozi wa kanisa. Chanzo kikubwa ni hekima ya Mungu kukiukwa na kufuatwa hekima ya kibinadamu. Ni nani hasa anamiliki kanisa na kuogopwa na kila muumini?  JE Ni Mungu, Mchungaji, Mwalimu, Askofu, Mtume, Mwinjilisti au Nabii?.

Mungu ni wakuofiwa kuliko wote wanaozungumzwa kulingana na Zaburi 89:7, viongozi ndio waliosajili Madhehebu katika wizara ya mambo ya ndani, na ndio wana Leseni. Lakini Yesu amesajili ROHO zetu mbinguni. Alitufia na kutununua kwa uweza wa Damu yake. 1Kor 6:20 na ndio Mwenye mbingu na sio viongozi, ila hekima ya Mungu huitajika katika kuishi na viongozi hao, kwa kuwa pamoja na yote hayo Neema ya Mungu huambatana nao.

Viongozi wengi leo makanisani hutaka kuwamiliki waumini, hivyo kwa kufanikisha hilo huamua kuwateuwa viongozi watakao kuwa chini yao wenye nguvu kidogo ya kuwajenga waumini na kuukosoa uongozi , na mara nyingine baada ya kuteuliwa, hatupaswi hufanya kazi ya  na kutetea maslahi binafsi ya watumishi hao, na bali kwa ajili ya kuujenga ufalme wa Mungu katika eneo hilo.


Viongozi makanisani wanasema sana kuhusu kujitenga mbali na mafarakano, wivu, chuki, lakini kukosa hekima ya Mungu ndiko zaidi kumezaa haya. Mungu amekipa heshima zaidi kile kiungo kilichopungukiwa ili kusiwe na faraka katika ya Mwili (kanisa) bali viungo vitunzane (1kor 12:24-25), ila kifanyikacho leo makanisani tunawapa heshima zaidi waliofanikiwa na kuwadharau wasiofanikiwa.


Elias S. Bilegeya.
+255-0765653985.
Dar-es-salaam.
Tanzania.

No comments:

Post a Comment