Home

Thursday, June 16, 2011

East Africa Music Awards

Kwa Mara ya Kwanza kabisa katika ukanda huu wa Afrika Mashariki kunakwenda kufanyika tuzo zijulikanazo kama EAMA`S (East Africa Music Awards) . Tuzo hizo zinajumuisha muziki wa aina mbali mbali ukiwemo muziki wa Injili kwa wanamuziki wa ukanda huu. Hosanna Inc inazigusia tuzo hizi kwa kuwa zimehusisha muziki wa Injili pia. Kikubwa ambacho kinahitajika ni kupendekeza jina la mgombea wa tuzo hizo kwa upande wa nyimbo za injili japokuwa siku zimebaki Chache.


Nchi zitakazoshiriki ni Kenya, Uganda, Tanzania, Rwanda, Burundi, DRC, Ethiopia and Sudan. Kazi za wanamuziki hao lazima ziwe zimefanyika kuanzia January 01, 2007 mpaka May 17,2011. Kilele cha tuzo hizo kinatarajia kuwa August 20th, 2011 katika jiji la Nairobi. 

Namna ya kupendekeza majina tembelea website ya EAMAS imeonyeshwa hapo chini. kwa uzoefu unaonyesha wenzetu wakenya kwenye tuzo zozote zinazohusu muzuki wa injili, wapenzi wa muziki huo pamoja na wadau huwa mstari wa mbele kuhakikisha wanawasapot wanamuziki wan nchi hiyo kitu ambacho watanzania hatukifanyi. Hivyo basi ni jambo la busara nasi kuwapendekeza wanamuziki toka Tanzania ili washiriki.

ANGALIZO: Tuzo hizi ni ngeni na hakuna undani wa namna mambo yatakavyoendeshwa, hivyo ni muhimu  watumishi wa Mungu watakaoshiriki kujua mipaka ya ushiriki wao. Hii inatokana na kutojulikana wazi nani atakuwa mdhamini wa tuzo hizo (kampuni, na ni bidhaa gani zinazalishwa na kampuni hiyo)  ili mwishoni isilete shida kwenye Himaya ya Mungu wetu. Kwa kuwa ni Bora kutopata tuzo yeyote kuliko kupata tuzo isiyo na utukufu kwa Mungu wetu. Kwa undani wa habari hii visit
www.goldendreams.co.ke

No comments:

Post a Comment