Home

Saturday, June 18, 2011

Miriam Lukindo atua Mwanza tayari kwa Uzinduzi


Mwanamuziki wa nyimbo za injili Miriam Lukindo pamoja na Upendo Nkone wamewasili jijini Mwanza tayari kwa ajili ya Uzinduzi wa Album ya Mriam iitwayo Ni Asubuhi. Akiongea na Hosanna Inc mara baada ya kufika Mwanza Miriam amesema wako Mwanza kwa sababu moja kubwa Kumsifu na Kumwabudu Mungu.

“ Tumekuja Kumsifu na kumwabudu Mungu katika jiji la Mwanza LIVE”,alisema Miriam. Timu yangu nzima kutoka Dar itakuwepo kuhakikisha hakuna Play Back. Watu wa kuniback kwenye Vocal, Drumist wangu Kapama, na wapiga vyombo watakuwepo siku hiyo.

Uzinduzi huu wa Miriam Umedhaminiwa na Haak Neel Production ambao watarecord Live video ya tamasha hilo lililopangwa kufanyika jumapili hii katika uwanja wa ccm Kirumba kuanzia saa nane mchana.

Miriam Lukindo akiwa jijini Mwanza

Miriam akifanya mahojiano na wadau wa Hosanna Inc

Miriam akiwa na wadau  John kushoto ambaye ni mratibu wa tamasha , Addo Nzwalla wa Kwa Neema FM pamoja na Bro Lonely Nzalli ambaye ni mratibu msaidizi


No comments:

Post a Comment