Home

Thursday, June 2, 2011

Filamu mpya ya Jenipher Mgendi Kuingia sokoni Mwezi Huu

Jenipher Mgendi
Mwanamuziki maarufu wa muziki wa injili nchini Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla Jenipher Mgendi, mwezi huu wa sita 2011, anatarajia kuiingiza sokoni Filamu yake ijulikanayo kama TEKE LA MAMA - N0 2. Filamu hii ni Muendelezo wa Filamu ya Teke la mama No 1.



Filamu hiyo yenye Lengo la Kufundisha na Kuelimisha jamii kuhusu ustawi wa Familia, imewahusisha wasanii mbalimbali akiwemo Lucy Komba, Christina Matai, Bahati Bukuku, Godliver Vedastus, Jenipher Mgendi mwenyewe na  na wasanii wengine wengi.



Mgendi ni mmoja kati ya watumishi wa Mungu nchini walioamua kujihusisha na utoaji wa Filamu kama njia nyingine ya kumtangaza Kristo. Baadhi ya watumishi wanaojihusisha na Filamu ni Pamoja na Upendo kilahiro, Sarah Mvungi, Pastor Harris Kapiga, Mc Luvanda, na Bahati Bukuku.

No comments:

Post a Comment