Home

Wednesday, July 13, 2011

Askofu Kakobe achaguliwa tena kuliongoza kanisa la Full Gospel Bible Fellowship


Askofu Zakaria Kakobe
Askofu mkuu wa kanisa la Full Gospel Bible Fellowship(FGBF) askofu Zacharia Kakobe amechaguliwa kuliongoza tena kanisa hilo askofu. Kakobe ambaye ni muanzilishi na mbeba maono wa kanisa hilo, amechaguliwa kuliogoza kanisa hilo katika uchaguzi uliofanyika mjini Dodoma wiki moja iliyopita.

Katika uchaguzi huo uliohudhuriwa na jumla ya wachungaji 450 wa kanisa hilo kutoka mikoa yote ya Tanzania, Askofu kakobe alipita bila kupingwa. Msimamizi wa uchaguzi huo ambaye ni Askofu wa kanisa hilo jimbo la Iringa. 

Askofu Nathaniel Meshak ambaye pia ni katibu mkuu wa kanisa hilo alisimama na kuwataka wajumbe wanaotaka kuwania nafasi ya uaskofu mkuu wajitokeze ila hakuna aliyejitokeza isipokuwa Askofu Kakobe pekee.

Kwa mantiki hiyo Askofu Zakaria kakoke alipita pasipo kupingwa baada ya wajumbe wote wa mkutano kukubaliana kuwa Mchungaji Kakobe aendelee na wadhifa huo. Hosanna Inc inamtakia kila la Kheri Mtumishi kakobe katika kulipeleka kanisa la Mungu pale ambapo Mungu mwenyewe analitaka lifike.

No comments:

Post a Comment