Home

Tuesday, July 12, 2011

Hosanna Inc yapata tuzo ya Blog Bora ya Dini nchini Tanzania


Ndugu wapenzi na wasomaji wa Blog Hii ya Hosanna Inc kwa niaba ya Timu nzima ya Hosanna Inc, tunapenda kumshukuru Mungu sana kwa kuiwezesha Blog hii kuchukua tuzo ya Blog bora ya Dini hapa nchini. Katika tuzo hizo zijulikanazo kama Tanzania Blog awards zilizofanyika jumapili iliyopita na matokeo kutangazwa jana jumatatu. 

Hosanna inc imeshika nafasi ya kwanza katika kategori ya BLOGS ZA DINI. Matokeo ya tuzo hizo unaweza kuyaona vizuri kupitia www.Tanzanianblogawards.com
Japokuwa hatukuweza kuwajulisha wasomaji wetu juu ya uwepo wa tuzo hizo na ushiriki wetu kwa kuwa tulipendekezwa na hatukujua undani wa tuzo hizo. Tulipowauliza wadau mbalimbali wa injili walituambia haina shida hao jamaa endeleeni nao. Matokeo yalipotoka yametupa picha kuwa kuna watu ambao walifuatilia kwa namna moja au nyingine na kutupigia kura.
Tunashukuru sana kwa wote waliotupigia kura. Tunaomba ieleweke kuwa blog hii lengo lake sio kushindana japo imetokea, bali lengo lake ni kuujenga na kuuimarisha mwili wa Kristo hapa nchini na Duniani kwa ujumla.
Hosanna Inc inapenda kutoa shukrani kwa watu wote ambao kila kukicha wamekuwa wakihakikisha blog hii inasonga mbele. Wapo wengi ila shukrani za pekee ziwaendee Pastor Emmanuel Fabrick, Bro Kelvin Nyanja Poti, Bro Samuel Sasali toka blog ya www.Samsasali.blogspot.com, Dada Mary Damian toka blog ya www.StrictlyGospel.worldpress.com, pamoja na blog ya Sayuni.
Hawa wote walitukaribisha na walitutia moyo wakati tunaanza, na mpaka leo kama watendakazi katika himaya ya Kristo wamekuwa wakitupa ushirikiano wa pekee Mungu awabariki . Kama Hosanna tunaamini kuwa sisi sio bora kuliko blogs nyingine, kwa kuwa aliye BORA ndio Hosanna Inc kila siku inamtangaza naye ni YESU KRISTO Pekee.
Kwa mujibu wa website ya Tuzo hizo Matokeo ya kategori hiyo ni kama ifuatavyo.
Best Religion Blog
http://hosannainc.blogspot.com/                      20.88%
http://nyimbozadini.blogspot.com/                    18.68%
http://zanzibarislamicnews.wordpress.com/    16.48%
http://christianceleb.blogspot.com/                   15.38%
http://strictlygospel.wordpress.com/                 10.99%
http://mtangazaji.blogspot.com/                         7.69%
http://kabulageorge.blogspot.com/                    5.49%
http://sayuni.blogspot.com/                                 4.4%

2 comments:

  1. Kwa heshima na taadhima, kaka nakupongeza, zaidi ya yote penye nia pana njia, kama hakuna njia tengeneze njia. Big Up sana

    ReplyDelete
  2. Big up kijana wangu!keep it up for the Glory of our LORD JESUS CHRIST!KPM

    ReplyDelete